KESI YA MAUAJI INAYOMKABILI PAPAA MSOFE YAZIDI PIGWA KARENDA, ARUDISHWA TENA RUMANDE
KESI ya mauaji
inayomkabili mfanyabiashara maarufu Marijan Abubakar ‘Papa Msofe’ na
mwenzake imeendelea kupigwa kalenda, baada ya upande wa mashitaka kudau
upelelezi haujakamilika.
Pia, umedai jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) na kesi itatajwa Machi 25, mwaka huu.
Msofe na Makongoro Nyerere wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya Onesphory Kitoli, jana walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa.
Wakili wa Serikali Leonard Challo alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na jalada la kesi hiyo liko kwa DPP kwa hatua zaidi.Msofe na mwenzake walirudishwa rumande.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni