Kampuni ya mbunifu mkubwa wa mavazi nchini Tanzania Sheria Ngowi imeanzisha ya ulipaji wa ki elektroniki kupitia kadi maalumu za Visa, Master na Union pay ili kurahisisha ulipaji kwa wateja wake na kuondokana na adha za kubeba fedha wakati wa malipo.

Akiongea wakati wa mafunzo yaliyo tolewa na benki ya CRDB jana makao makuu ya kampuni hiyo Masaki
jijini dar es salaam, Afisa mahusiano kampuni hiyp Kelvin Lyimo alisema, huduma hiyo itasaidia katika kufanya malipo kwa urahisi na uhakika zaidi kwa wateja wao wafikapo katika ofisi hiyo.
Lyimo alisema hudauma hiyo pia ita wasaidia wateja wao kupunguza usumbufu wakupanga foleni kwenye ma benki kwa muda mrefu wakati wakulipia fedha na hivyo kuwapa wateja nafasi ya kuendelea na shughuli zingine za kimaendeleo.
Naye meneja chaps wa benki ya CRDB, Getrude michael alitoa rai kwa ma kampuni mengine kuiga mfano huo ili kurahisisha shughuli za malipo ya kifedha katika ufanyaji biashara .
Kampuni ya sheria Ngowi ni kampuni iliyo anzishwa mwaka 2008 na Sheria Ngowi ambaye amejipatia heshimakubwa nchini Tanzania na ulimwengu mzima kutokana na ubunifu wa kipekee wa mavazi ya kiume , na ya kikie pamoja na sare za makampuni mbali mbali Nchini na Nnje ya Nchi ya TANZANIA.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni