Ali Kiba Atangaza Kuanza Mwaka na 'Surprise'
Ali Kiba akiwa katika ofisi za EATV alipofanya ziara maalum siku ya Jumamosi Tarehe 09/01/2015
Kiba a.k.a Fundi ameiambia eNewz kuwa amefurahi kuona mashabiki wamempokea tena vizuri na kumpa nguvu ya kuendelea kuwatengenezea kazi zenye viwango vya kimataifa.
Kuhusiana na kiu ya mashabiki wengi kujua Kiba mwaka huu ana uanzaje, na vilevile kuhusiana na kolabo za kimataifa, Kiba amesema mipango imeshasukwa, akiwa amejipanga kutoa kazi kwa mtindo wa Bumper 2 Bumper, mpango utakaoanza mwezi huu wa Januari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni