vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Ijumaa, 22 Mei 2015

Mose Iyobo: Aunt Ezekiel Amekwamisha safari ya London


Staa maarufu wa filamu Bongo Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moses Iyobo.

Dansa wa mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ Mose Iyobo, ambaye pia ni mpenzi wa staa maarufu wa filamu nchini Tanzania,Aunt Ezekiel, amefunguka kuwa hajajumuika na dansa wenzake kwenda jijini London, Uingereza kutokana na hali ya mpenzi wake.

Mose, amesema kuwa alishindwa kujumuika na wenzake akihofia hali ya mpenzi wake na kudai kuwa anapenda kuwa na mrembo wake karibu hadi hatua za mwisho za kujifungua kwake.

Ameongeza kuwa anashindwa kwenda mbali sana kutokana na hali ya mpenzi wake kwa kuwa anakuwa na wasiwasi sana hivyo hata London, ameshindwa kwenda kwani anatamani kuona hatua kwa hatua ya mpenzi wake hadi kumpata mtoto wao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni