Kwa mujibu wa majirani wa staa huyo, nyumba hiyo imejengwa katika njia ya maji (mkondo), jambo ambalo hakulielewa hapo mwanzo, kwani ndiyo sababu kubwa iliyodondosha ukuta wa uzio wake muda mfupi baada ya Diamond kuhamia wiki kadhaa zilizopita.
“Kabla ya ujenzi, kiwanja hiki kilikuwa na njia kuu mbili za maji ambazo wakati wa mvua, zilikuwa zinatiririsha maji kuelekea bondeni, lakini baada ya ujenzi, nguvu ya yale maji yakadondosha ukuta.
“Sasa ukiacha ukuta uliobomoka mwanzoni, kuna njia nyingine ambayo inapitisha maji mengi zaidi ambayo inapita kwenye ukuta wake mwingine na tayari yameanza kuuchimba kwa chini. Mnaweza kuja kuangalia,” alisema jirani mmoja aliyekataa kutaja jina lake.
Waandishi wetu walifika nyumbani hapo na kumkuta fundi ujenzi akijaza kifusi nyuma ya ukuta uliovunjika mwanzo huku upande mwingine wa ukuta maji yakionekana kutiririka kwa kasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni