vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Jumatano, 10 Juni 2015

Aunt Ezekiel Atoboa Kuhusu Mzazi Mwenzie Mcheza Show Moses Iyobo


Aunty na Moses Iyobo
Staa wa Bongo Movies, aunt Ezekiel amaeamua kuatoboa kuhusu baba mtoto wake Moses Iyobo  kwa kudai kuwa ndiye baba halisi wa mwanae na anampenda kwa dhati  todauti na baadhi ya watu  wanavyomtafsiri kuwa yeye ni mpenda hela!

Aunt aliyaongea hayo katika mahojianao maalumu na kusema kuwa kama kuna watu wanaomtafsiri kama yeye ni mpenda hela na hawezi kujkaa na Iyobo  kiatendo  ambacho sio cha kweli katika moyo wake kwani anachohitaji kutoka kwa Iyobo ni mapenzi tu.

“Nataka ni weke wazi kuwa nimejianda na nimejipanga kuishi na Iyobo au baba cookie  kwa sababu ambazo najizua mimi na sikushawishiwa na mtu mataka watu waanze kunifuatilia  kuhusu mapenzi haya naamini mapenzi  yangu yako  kwake  kama ilivyo kwa mtu mwingine,” alisema  Aunt

Aliendelea kuongeza kuwa unaweza kuwa  na mpenzi mwenye pesa  lakinI maudhi ya kila siku katika maisha yakawa mengi jambo ambalo linaondoa raha kabisa

‘ Ili mradi mpenzi wangu anahele  ya kukidhi shida zetu haijalishi  watu wanasema nini, ninachotaka ni mapenzi ya dhati tu kutoka kwetu  hayo mengine waache watu waongee mpaka wachoke,”  alisema Aunt.

Hata  hivyo Aunt aliesema kuwa  hata mimba yake  haikuingia kwa bahati mbaya  bali iliingia  kwa makusudi ndio maana hakuwa na presha  katika makuzi ya mimba hiyo.

Kama hiyo haitoshi  Aunt aliongeza kuwa  anajua kuwa Iyobo alikuwa na mwanamke aliezaa naye  lakini sio mkeo sasa kama kuna mtu anadai amechukua mume wa mtu ajue kuwa nay eye ni mke wa mtu vilevile.

“Sijaiba mume wa mtu Iyobo hajaoa jamani tuacheni tufanye yetu naamini  kila kitu kinaendelea maisha  nalea mwanangu  bila ya matatizo  na sihitaji  bifu na mtu,” aliweka wazi Aunt

Gazeti la KIU

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni