vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Jumatano, 17 Juni 2015

Baba Haji, Lemutuz Watifuana, Kisa Mchango wa Harusi


Staa wa Bongo Movies, Adam Haji ‘Baba Haji’ amemtolea uvivu ‘The King Of All Bongo Social Media Network’ Lemutuz kutokana na tukio la udhalilishaji  alilolifanya dhidi yake!

Lemutuz ambaye amezoeleka kwa kutoa hisia na mtazamo wake juu ya mambo mbali mbali mtandaoni, mapema wiki iliyopita alimnanga Baba Haji kupitia ukurasa wke kwenye mtandao wa instagram akidai kuwa  amekuwa akisumbua kuhusu michango ya harusikiasi cha kubadili staili ya kudai michango hiyo.

Kutokana na kitendo hicho Baba Haji alishindwa kuvumilia  na kuamua kuandika waraka wa kumjibu kumjibu Lemutuz kupitia mtandao huo huo wa instagram ambapo wasomaji wengi walimuunga mkono na kumshambulia Le Mutuz

Waraka wa Baba Haji ulisema hivi;

Harusi ni jambo la kheri sana kwa wenye kujua, yaani kwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliowapa hali ya kulijua hilo! Kiukweli hatuwezi kubisha kwamba ktk Africa watu sote hushauriana na kuchangiana kufanikisha fanction (shughuli) na sio Mahari au maulidi ambayo nimefanya ili kubariki ndoa yangu, na imekuwa kawaida sana kwa miaka ya zamani kabla kuzaliwa kwangu 1980 na hadi sasa.

Wajinga (Kina Lemutuz) wasiojua wenye hila na gilba na inda hupotosha sana watu kwakua tu wao wazazi wao walituibia pesa za mlipa kodi na kwenda kusoma USA au Ulaya na eti wakachukua mila za huko ambazo ni za kiyunani kwa udhalilishaji dhidi yangu eti nilikusumbua kwa simu kukuomba mchango na kisha nikabadili style ya kukufuatilia unichangie mtu mzima ovyo muongo sana wewe huna utu kabisa umejaa nafsi ya kizembe na ujinga uliopitiliza.

Sidhani kama una akili timamu na sidhani kama unalilinda jina la mlezi wako abilisi wa mguu mmoja chago mtembea upande upande.

Baada ya Baba Haji kuweka waraka huu, maoni ya wasomaji wengi yalimshambulia Lemutuzi kwa kile alichokifanya na kumtuliza Baba Haji kwa udhalilishaji aliofanyiwa na mtanzania mwenzake anayejifanya kakulia Marekani.

Picha: Baba Haji akiwa na mkewake siku ya harusi yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni