vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Alhamisi, 4 Juni 2015

Jinsi mbinu za kusafirisha ‘unga’ zinavyofichuliwa


Wakati vyombo vya usalama duniani vikitumia kila njia kuhakikisha kuwa biashara ya dawa za kulevya inakomeshwa, wasafirishaji nao wamekuwa wakibuni mbinu mpya kila siku.

Hata hivyo, mbinu za wafanyabiashara hao zimekuwa zikifichuliwa kwa kutumia vifaa maalum, kama kamera na mbwa wanaokuwapo kwenye viwanja vya ndege na mipakani. Vifaa hivyo huweza kuona au kunusa vitu vilivyofichwa ndani ya mabegi, makopo  hata tumboni.

Gazeti la The Telegraph la Uingereza limekusanya baadhi ya picha zinazoonyesha mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wahalifu kusafirisha ‘unga’. Baadhi ya picha zinaonyesha dawa za kulevya zikiwa ndani ya maparachichi, mananasi, tumboni mwa watoto wa mbwa waliokuwa wakisafirishwa.

Pia, baadhi ya wasafirishaji hao waliibuka na mbinu mpya za kujifunga tumbo la ujauzito wa bandia lililosheheni cocaine, huku wengine wakijifunga mwili mzima mifuko ya dawa hizo.

Ritchie Tabatha Leah, raia wa Canada, alinaswa kwenye Uwanja wa ndege wa Bogota Septemba mwaka 2013 akiwa amejifunga tumbo la bandia ili aonekane mjamzito, lakini alipopekuliwa muda mfupa kabla hajaingia kwenye ndege alikutwa na kilo2 za dawa aina ya cocaine.

Genge la wauza dawa za kulevya waliwafanyia upasuaji watoto wa mbwa kisha kuwabebesha dawa za kulevya aina ya heroine. Hata hivyo, mpango huo ulivurugika baada ya polisi kuubaini kupitia kamera maalumu.

Picha za X-ray zilionyesha mifuko iliyowekwa dawa za kulevya tumboni mwa mmoja wa abiria aliyenaswa katika mmoja ya mipaka ya Uingereza wakati akijaribu kuingiza ‘mzigo’ huo.

Askari wa Colombia waliokamata nyambizi kwenye mji wa Timbiqui baada ya kuihisi imebeba dawa hizo, walibaini ilikuwa imebeba tani 8 mwaka 2011. ‘Unga’ huo ulikuwa ukipelekwa Mexico.

Mtu mwingine alikamatwa na maafisa wa forodha kwenye Uwanja wa Ndege wa Kabul nchini Afghanstan akiwa amejiviringisha mwilini dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 7 Juni 2007.

Polisi nchini Hispania walifanikiwa kukamata kilo 200 za cocaine zikiwa zimefichwa ndani ya nanasi ambalo lilikuwa limesafirishwa kutoka kutoka Marekani. Nanasi hilo lilipatikana ndani ya moja ya makontena 10 yaliyokuwa yamewasili kutoka bandari ya Algeciras.

Raia wa Chile mwenye umri wa miaka 66 aliyekuwa amevaa bandeji ngumu inayotumika kufunga mtu aliyevunjika, alikamatwa kwemye Uwanja Ndege wa Barcelona mwaka 2009 baada ya kubainika kuwa hakuwa mgonjwa bali alikuwa amebebwa dawa za kulevya.

Parachichi lililosheheni dawa za kulevya aina ya cocaine likiwa limepasuliwa baada ya polisi kulitilia shaka.

Wakati mwingine huonekana kama mayai, lakini ukweli ni kwamba hayana ladha ya mayai. Mtu aliyebeba mzigo huo alikamatwa na maofisa uhamiaji wa Marekani. Mtu huyo, Esteban Galtes alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Los Angeles akiwa na cocaine.

Mwanasesere aliyekuwa ametumwa kupeleka kitu kama zawadi nchini Australia kutoka Sydney mwaka 2007, alinaswa na maofisa wa kupambana na dawa za kulevya baada ya kubainika dawa za kulevya zilikuwa zimefichwa ndani yake.

Mfuko wa James Bettridge uliokuwa na cocaine ulikamatwa na maofisa wa polisi Agosti mwaka jana nchini Uholanzi muda mfupi baada ya kuwasili kutoka Ufaransa.

Tani 15 za dawa za kulevya aina ya bangi zilikamatwa baada ya polisi kuzing’amua ndani ya kontena.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni