vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Ijumaa, 19 Juni 2015

Mrembo FAIZA ALLY Awaomba Radhi Watanzania......


Imelda Mtema
MZAZI mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Faiza Ally, hivi karibuni katika tuzo za KTMA aliwaacha watu midomo wazi baada ya kutinga na kivazi kilichoacha sehemu kubwa ya makalio yake nje na kuzua minong’ono katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Amani kwa kuonekana kujutia kitendo kilichotokea, Faiza alisema kuwa ile nguo aliishona ikiwa imeziba sehemu yote ya nyuma japokuwa ilikuwa imechanwachanwa lakini hakuwa na nia ya kuacha sehemu ya makalio yake nje.

Akiendelea kuzungumza alisema kuwa, siku alipokuwa akienda kwenye tuzo alikuwa peke yake kwenye gari hivyo alivyoinuka ndiyo ile nguo ikapanda bila kufahamu.“Jamani siwezi hata siku moja kujiachia hivyo naomba Watanzania wanisamehe,” alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni