vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Jumanne, 11 Aprili 2017

Hivi Ndivyo Naibu Spika Alivyokataa Kata Kata Kuruhusu Bunge Kujadili Suala la Utekaji wa Kina Roma..Akidai Jambo Hilo Halina Maslahi kwa Nchi...!!!

MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), amedai kupewa taarifa na mawaziri kuwa muda wowote anaweza kuuawa na kikundi maalumu kinachoendesha utekaji nchini.
Aidha, Bashe amedai kuwa mbali na yeye kuwa katika hatari hiyo, pia ameambiwa na mawaziri hao wa serikali kuwa kuna wabunge wengine 10 ambao wanawindwa na kikundi hicho na wametahadharishwa 'kuwa makini barabarani'.
Bashe (41), aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana asubuhi aliposimama na kukiomba Kiti cha Spika kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili hoja ya dharura akitumia Kanuni ya 47(1),(2)na (3) vya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016.
Huku akiungwa mkono na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) na kushangiliwa na baadhi ya wabunge, Bashe alisema kumekuwa kukitokea matukio ya sintofahamu yanayowahusu wabunge na raia wa kawaida yanayoendeshwa na kikundi hicho ambacho alidai kinatoka idara nyeti serikalini.
Katika kujenga hoja yake, Bashe alisema Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku (CCM), mbunge wa zamani Mkuranga mkoani Pwani, Adam Malima (CCM), msanii Roma Mkatoliki na yeye mwenyewe ni miongoni mwa watu waliowahi kutekwa huku akikumbushia pia madai ya kupotea kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Aliliomba shughuli za Bunge ziahirishwe ili wabunge wajadili jambo la dharura ambalo limekuwa likitokea kwa muda mrefu katika nchini.
"Miongoni mwa watu waliowahi kutekwa ni Mheshimiwa Musukuma (Joseph Kasheku), Mheshimiwa Bashe kwenye mkutano mkuu wa CCM, ndugu Malima, Ben Saanane amepotea... (makofi), juzi amepotea Roma Mkatoliki," alisema Bashe huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge kwa kugonga meza.
Alisema zaidi: "Nasema ni jambo la dharura kwa sababu hawa ni wale ambao wanafahamika. Hatujui Watanzania wangapi hawafahamiki katika ngazi za chini.
"Na zipo taarifa ambazo binafsi nimezipokea kutoka kwa baadhi ya mawaziri, wakinitahadharisha mimi binafsi kwamba 'Bashe kuwa makini, wewe ni mmoja kati ya wabunge 11 ambao wamewekwa katika 'list' (orodha). Mkikaa barabarani vibaya, mnaweza kupoteza maisha yenu'.
"Nasema jambo hili ni dharura kwa sababu kikundi hiki kilichomo ndani ya idara ya ... (alitaja idara nyeti), ambacho kimeamua kuchukua mamlaka haya ya kuteka watu, kinaharibu heshima ya serikali yetu, kinaharibu heshima ya chama changu ambacho mimi na wabunge wenzangu wa CCM, tuliomba ridhaa ya kutaka kuwaongoza Watanzania na siyo kuwahatarishia maisha yao."
Bashe alimuomba Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, kuruhusu jambo hilo lijadiliwe na wabunge na ikiwezekana chombo hicho cha kutunga sheria kiunde kamati maalumu ya kuchunguza jambo hilo.
Bashe pia alimuomba Naibu Spika kutumia mamlaka yake kuiagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Usalama na Mambo ya Nje kufanya kazi changamoto hiyo na kulipatia Bunge taarifa kwa ajili ya usalama wa nchi.
"Hali ya nchi siyo salama, Watanzania wana taharuki, Watanzania wanajadili mambo haya katika mitandao na 'there is no statement' (hakuna kauli) toka serikali.
Waziri wa Mambo ya Ndani..." Bashe alisema huku akikatishwa na Naibu Spika ambaye alimtaka aketi ili Kiti cha Spika kiangalie Kanuni ya 47 inaeleza nini kuhusu madai yake.
Kabla ya kutoa uamuzi wa Kiti kuhusu madai ya Bashe, Naibu Spika alitoa nafasi kwa Sugu kueleza hoja yake bungeni baada ya mbunge huyo kusimama na kuomba kupewa nafasi ya kuwasilisha hoja ya dharura bungeni.
Akitumia Kanuni ya 47, Sugu aliunga mkono hoja ya Bashe kwamba Bunge liahirishe shughuli zake za jana na kujadili hoja ya dharura ya kadhia ya utekaji na kupotea kitatanishi kwa watu nchini.
"Taifa limekuwa gizani kwa utamaduni mpya uliozuka wa kuteka watu, utamaduni ambao si wa kwetu, ni utamaduni wa kimafia, utamaduni ambao kwa mara ya mwisho kwenye mipaka ya Bara na visiwani, tuliusikia alipotekwa Mzee Kassim Hanga kule Zanzibar miaka hiyo," Sugu alisema.
"Lakini tangu kipindi hicho haujakuwapo tena. Toka operesheni hii ya kuteka watu nyara ianze, kila anayehusika na usalama likiwamo Jeshi la Polisi, 'always' (mara kwa mara) wanasema 'hatujui, hatujawaona kwenye vituo vyote'.
Nchi inabaki kwenye tahayari, kapotea Ben Saanane, mara miili sita, saba imeopolewa kwenye Mto Ruvu ikaenda kuzikwa bila kufanyiwa 'post-mortem' (uchunguzi) kwa amri ya ambaye hatujui ni nani.
"Bashe alitekwa, Nape (Nnauye) alitekwa, akaokolewa na Maulid Kitenge, vinginevyo pengine angekuwa ametekwa, hakuna mtu aliyezungumza kitu."
Kutokana na changamoto hiyo mpya nchini, Sugu alimshauri Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kuachia ngazi ili kulinda heshima yake kama kweli bado ana matumaini ya kuwa Rais wa Tanzania.
"Waziri wa Mambo ya Ndani yuko kimya mpaka najiuliza kama anabanwa kiasi hicho, huyu ni mtu 'potential' (muhimu) ambaye alifikia hatua ya kugombea urais na bado ana 'future'," Sugu alisema.
"Kwanini asijiuzulu, akalinda heshima yake kuliko kukaa kwenye 'mess' (aibu)? Alihoji Sugu. "Kujiuzulu ni utamaduni mzuri.
Mzee (Alhaji Ali Hassan) Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani miaka hiyo, mwaka '76, ikatokea messy (kuboronga), 'aka-bounce back' (akarejea), miaka ya '80 akaja kuwa Rais wa nchi hii.
"Ndugu yangu Mwigulu, nikushauri kama hushirikishwi, mambo yanafanyika, hamna mtu anakuja na majibu.
"Lakini juzi baada ya kutekwa Roma Mkatoliki, tumepata mwanga. Yupo mtu Dar es Salaam alituambia anajua Roma aliko na angerudi kabla ya Jumapili.
"Kama Waziri Kivuli (wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), nikatoka Jumamosi na 'ku-demand' (kuagiza) kwamba aachiwe siku ileile na akaachiwa, nashukuru Mungu. Sasa basi, hatujui nani 'next' (anayefuata) atatekwa. Yawezekana Sugu ingawa mimi 'I don't care much' (sijali) kwa sababu Mbeya wataziba nafasi yangu.
"Lakini Naibu Spika 'it could be you' (yaweza kuwa wewe). 'It is the war' (ni vita), 'no body is safe' (hakuna aliye salama. Kwanini Bunge hili lisijadili na hatimaye limlazimishe Bashite kama alivyojua kwamba Roma Mkatoliki yuko wapi na angemrudisha Jumapili, tumlazimishe sasa Bunge hili tujadili na baadaye tumlazimishe Bashite atutajie aliko Ben Saanane na atutajie kwamba ili miili iliyotupwa Ruvu na kuzikwa haraka haraka bila kufanyiwa 'post-mortem' ni ya kina nani kwa sababu huyu anaonekana anajua undani wa mambo haya."
KULIPATIA UFUMBUZI
Akijibu maombi ya wabunge hao, Naibu Spika alikataa kuruhusu jambo hilo kujadiliwa bungeni kwa kupitia utaratibu wa hoja ya dharura kwa kuwa vyombo vya sheria vinaweza kulipatia ufumbuzi.
Dk. Acskon alisema jambo la dharura linaloweza kusababisha kuahirishwa kwa shughuli za Bunge kulijadili ni lile lenye maslahi kwa umma na iwapo utatuzi wake unategemea zaidi ya utekelezaji wa kawaida wa sheria.
"Waheshimiwa Bashe na Sugu wameeleza kwa kirefu kuhusu jambo ambalo limetokea hapa na pale, lakini pia tumeliona kwenye vyombo vya habari na tumelisoma," Dk. Ackson alisema.
"Maelezo yao kwa ujumla yanahusu mambo ambayo yanawapata wananchi ambayo watu kadhaa wametajwa kama mifano kwamba wamekuwa wakitekwa ama wamekuwa wakikamatwa.
"Sasa, nadhani wote tunafahamu matakwa ya Kanuni ya 47, hili jambo la hawa watu kukamatwa ama kutekwa kwa sababu sasa hata wale waliokamatwa, na wao wamewekwa kwenye kundi la kutekwa. Sasa sijui kama tunaweza kuyatenganisha haya mambo mawili; nani amekamatwa na nani ametekwa?
"Lakini maelekezo yaliyotolewa kwa kirefu ni kwamba wakati mwingine mtu akiwa haonekani, polisi ndiyo sehemu ya kwanza ambayo inaulizwa na yapo mazingira polisi haijatoa maelezo kwamba hawa watu wako wapi na mifano imekwishatajwa.
"Mheshimiwa Bashe amekwenda mbali zaidi akisema kwamba kipo kikundi ambacho kinafanya kazi hiyo.
Na Mheshimiwa Joseph Mbilinyi na yeye ameeleza kwamba hili jambo sasa limekuwa kama utamaduni kwa maana ya kwamba linatokea kila wakati na akaenda mbele zaidi na kumshauri Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Nchemba) kwamba aweze kujiuzulu akiona inafaa.
"Kanuni ya 47 huwa ni lazima isomwe pamoja na (Kanuni ya) 48 kwa sababu 48 ndiyo inayoweka masharti ya matumizi ya Kanuni ya 47.
Sasa kwa kuwa Kanuni ya 48(4) nitaisoma, inasema hivi 'jambo lolote litahesabiwa kuwa ni lenye maslahi kwa umma iwapo utatuzi wake unategemea kuwa zaidi kuliko zile za utekelezaji wa kawaida wa sheria peke yake.
"Masuala haya yaliyoulizwa na Mheshimiwa Bashe na pia yaliyoulizwa na Mheshimiwa Mbilinyi yako chini ya utaratibu wa kisheria na Bunge hili litashughulika na mambo ambayo ni yenye maslahi ambayo sheria haina uwezo wa kuyatolea majibu.
Kwa sababu hiyo, sitalihesabu hili jambo kwa mujibu wa Kanuni ya 47(4) kwamba ni jambo la dharura lakini ni jambo ambalo utaratibu wa kawaida wa kisheria unaweza ukafanya kazi. Hayo ndiyo majibu yangu kuhusu matumizi ya Kanuni ya 47.
Matukio ya kupotea, kutekwa na kuuawa kwa wanasiasa nchini ni nadra, ingawa Juni 12, mwaka jana, chama cha ACt-Wazalendo kilidai kiongozi wake mkuu, Zitto Kabwe, alikuwa hajulikani alipo kwa zaidi ya saa 12 huku akiwa anasakwa na Jeshi la Polisi.

Zaidi ya Habari...Vitisho Vyazidi… Mama Aikimbia Nyumba, Amwambia Nay Aache Muziki

WAKATI msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, akiende­lea kusaka faraja ya moyo kutokana na kudai kuwa amekuwa akikabiliana na vitisho, mama yake mzazi ameamua kuondoka ny­umbani kwake akihofia ku­uawa.
Nay aliingia kwenye mgogoro na serikali kutokana na wimbo wake wa Wapo uliosababisha ashikiliwe na jeshi la polisi pamoja na wimbo huo ku­fungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) lakini al­iokolewa na kwa amri ya Rais John Magufuli.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Nay amesema pamoja na tamko la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, kutoka kwa rais, kuruhusu wimbo wake uchezwe kote, ameende­lea kuwa na vitisho kila kukicha kutoka kwa watu asiowafamu.
“Ninaishi kwa mashaka makubwa, tangu nilipoachia wimbo huu, maana kumekuwa na mfululizo wa kupigiwa simu na meseji za watu wakinitishia maisha jambo ambalo limepelekea hadi mama yangu kuamua kuhama ny­umbani kwangu na kurudi kwake.
“Kabla sijatoa wimbo huu nilikuwa naishi na mama nyumbani kwangu, lakini ameamua kuondoka kufuatia kutishiwa maisha kila kukicha, lakini baya zaidi vitisho hivyo vimenifanya mimi na mama kupishana mawazo am­bapo ameniambia niachane na wimbo huo, tena ikiwezekana niachane na muziki ili nifanye biashara zingine jambo ambalo sijam­kubalia.
“Nafikiri kutomkubalia kwangu dhahiri nahisi itakuwa ndicho kisa cha kuamua kuondoka na kurudi nyumbani kwake, napata tabu sana na wimbo huu, lakini naamini mimi ni mtu wa mi­simamao hivyo si­wezi kuachana na muziki kisa vitisho.
“Katika maisha hakuna jam­bo rahisi hasa kama wewe ni mpambanaji, vitisho kama hivi sitaki kuvipatia nafasi ya ku­niharibia maisha kwani mimi ninachokifanya ni kuwakilisha mawazo ya wazalendo wengi ambao imekuwa ni ngumu kila mmoja kufikisha maoni yake kwa jamii.
“Kuna watu wanadhani nilipoitwa na Mwakyembe nilienda kushikiwa akili ili ni­badili muziki wangu lakini ukweli ni kwamba, kule alikuwa akinipa ush­auri wa kawaida tu, hivyo hakuna jambo ambalo amenibadili­sha kwenye muziki wangu na nitaen­delea kupigania ninachokiamini ili nitimize ndoto yangu.
“Kifo kipo tu lakini wengi t u m e k u w a waoga wa ku­tangulia hasa ukifikilia jamii inayokuzunguka, Wapo imenikutan­isha na watu nisio­wafahamu, maana nakumbuka siku mbili nyuma zilizo­pita nilipigiwa simu na mtu nisiyemjua akidai anahitaji ku­fanya biashara na mimi hivyo nikaenda kuonana nae Ubungo.
“Huwezi kuamini ningekua muoga basi nisingemsikiliza maana baada ya kukutana alinitoa chemba na kuanza kunihusia juu ya kuachana na wimbo huo akidai watu wameji­fanya kunichunia lakini hakuna anayefurahishwa, hivyo kama nataka amani iendelee basi niuache na kingine akaniamia niwe makini kwani kuna watu wana nia mbaya na mimi.
“Kusema kweli nimeshatishwa sana lakini watu wanacho­takiwa kujua kama kifo kipo basi nitakufa kwa kuwatetea mamilioni ya mashabiki zangu, ila suala la kushikiwa akili au kubadilishwa gia yangu hapa halina nafasi,” anasema Nay.
Ikumbukwe kwamba mwishoni mwa wiki iliyopita Nay baada ya kutoka Dodoma, alikoenda kui­tikia wito wa waziri Mwakyem­be, alisema amefarijika kwa namna moja au nyingine hasa baada ya kukutana, kwani wali­pata muda wa kuketi na kuzun­gumza mambo mengi juu ya sanaa ya muziki.
Huku akimtaka kuwa makini na tunzi zake kwani zimekuwa na mfululizo wa maneno ya kuwa­gusa watu moja kwa moja hivyo awe makini kwani kuna wen­gine huwa si wavumilivu kwani asipojiahadhali wanaweza kuja kumdhuru kwa namna moja au nyingine.

Jumatatu, 10 Aprili 2017

Kiongozi Aliyetoza Faini Maiti Asakwa..!!!


Kiongozi wa kimila katika Kijiji cha Endagulda ameamriwa akamatwe baada ya kuitoza faini maiti.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Chelestino Mofuga aliagiza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kiongozi huyo.
Mofuga ametoa agizo hilo juzi kijijini hapo baada ya baadhi ya wananchi kulalamika kuwa, mzee wa kimila, Joseph Daniel aliagiza Gadii asizikwe hadi faini hiyo itakapolipwa.
Awali, kiongozi huyo wa kijiji aliagiza kulipwa faini ya ng’ombe mmoja kutoka kwenye zizi la marehemu Boay Gadii (42) kabla ya maziko yake ikielezwa kuwa alitengwa na jamii.

Mfumuko wa Waongezeka kwa Asilimia 1.4..Sasa Umefikia Asilimia 6.4..!!!

Kiwango cha mfumuko wa bei nchini kimepanda kwa wastani wa 1.4 kutoka asilimia 5 ilivyokuwa mwezi Februari hadi asilimia 6.4 kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini (NBS).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya sababu zilizochangia ongezeko hilo ni kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula ambapo vyakula vilivyopanda bei ni pamoja na mchele, sukari, unga wa mahindi, mtama, ndizi pamoja na mihogo mibichi.
Kufuatia ongezeko hilo, baadhi ya wakazi Jijini Dar es Salaam wametoa maoni yao na kutaja ukosefu wa kipato kuwa unaongeza ugumu wa maisha hasa kwa wafanyabiashara ambao wamelalamikia upungufu wa wateja sambamba na ushauri wa hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo.

Watuhumiwa Watatu Waitwa Marekani Kwa Tuhuma Za Biashara Ya Dawa Za Kulevya


Waziri wa Katiba na Sheria amewasilisha maombi  ya kuwasafirisha washitakiwa watatu akiwemo Ally Hatibu Hassan maarufu kama Shkuba  kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kujibu tuhuma za kusafirishaji dawa za kulevya.
Washitakiwa wengine ambao wanaungana na Shkuba ni Idd Mafuru na Lwitiko Emmanuel Adam.
Maombi hayo yamewasilishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya kifungu namba 5 (1) cha Sheria ya Usafirishaji wahalifu sura ya 368 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Katika maombi hayo upande wa waziri kupitia DPP wanaiomba mahakama hiyo isikilize ushahidi na itoe amri ya kuwahifadhi washitakiwa ndani wakiwa wanasubiri kibali cha Waziri huyo cha kuwasafirisha nje ya nchi kwa mashitaka hayo.

Vichwa vya Magazeti ya Leo 11/4/2017..!!! Magazeti ya Leo




Zitto: Nimetonywa Kuna Mpango wa Watu Saba Kutekwa Wakiwamo Mimi na Mawaziri Watatu...!!!!



Kama muelewavyo story za kuteka na kutaka kutekwa zimepamba moto na kila mtu hasa wabunge wanasema wanataka kutekwa.
janakwenye kipindi cha DW alitafutwa mbunge Zitto kuzungumzia hili swala kwanza aliulizwa kama ana taarifa ya bashe kusema kuna wabunge 11 wanatafutwa kutekwa akasema hana taarifa kamili na ni vigumu yeye kulielezea na alisema kuwa yeye binafsi alitonywa kuwa kuna watu saba nje ya bunge, wabunge na mawaziri watatu wanapangwa kutekwa....
Lakini Zitto aliulizwa una uhakika gani na vyanzo vyako kama havikudanganyi? alisema yeye ametonywa na ana haki ya kuchukua tahadhari.. hata hivyo aliulizwa mbona taarifa zake na mbunge wa Nzega zinakindhana mwenzie anasema watu 11 na yeye anasema watu 7 wakiwemo mawaziri? Zitto alijibu kwa kusema yeye hajui vyanzo vya bashe vilivyo mpa taarifa ila yeye ana vyanzo vyake hivyo siwezi jua vyanzo vya Mh Bashe.
Pia Mh Zitto aliulizwa kama anamjua muhusika wa utekaji huu akasema angekuwa anamjua asingelipiga kelele na wala isingekuwa mjadala tena...
Pia Mh Zitto alisema kuwa yeye kesho atawasilisha hoja bungeni kutaka waunde kamati maalum ya kuchunguza matukio hayo ya utekaji na lazima watu wawajibike
Source: DW(6:00-6:30 PM)