Batuli Aitikisa Ndoa Ya Mtunisy,
![]() |
| Batuli |
Star wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph "Batuli" anadaiwa kuitikisa
ndoa ya star mwenzake wa filamu Nice Mohamed "Mtunisy" ambaye waliwahi
kuwa wapenzi kipindi cha nyuma kwa miaka kadhaa kabla ya kumwagana. Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kwa
sharti la kutotajwa jina lake gazetini kilifunguka kuwa issue ya wawili
hao kuwa wapenzi siyo siri, kwani mara kadhaa wamekuwa wakijiachia
sehemu mbalimbali, huku mke wa Mtunis akinyetishiwa, jambo
lililosababisha migongano ndani ya ndoa hiyo.
"Mmechelewa kweli kujua! Leo ndiyo mnauliza kuhusu Mtunis na Batuli? Hao
ni wapenzi na penzi lao limenoga kwelikweli sasa hivi. Imefikia hatua
Mtunis na mkewe hawana maelewano mazuri. Nyumba ni kama inayumbishwa na
Batuli lakini Mtunis hataki kumwacha Batuli,” kilipasha chanzo hicho.
![]() |
| Mtunisy |
Kwa upande wa Mtunisy ambaye filamu yake mpya ya Jike Dume inaingia
sokoni tarehe 1 mwezi May alipotafutwa na mtandao huo na kuulizwa
alikana madai hayo kwa kusema "Kwanza nani amekuambia kuwa mimi natoka
na Batuli? Yule ana mtu wake na mimi nina ndoa yangu. Sikia kaka, katika
kipindi ambacho ndoa yangu ina amani ni hiki, sitaki kabisa haya mambo.
Mtakuja kusababisha Batuli agombane na mumewe kisa mimi"
Batuli alipotafutwa kwa njia ya simu, alikuwa msikivu muda wote
alipoelezwa kuhusu madai hayo, mwishoni akajibu kwa mtindo wa kuuliza:
“Kwanza nikuulize, Mtunis ni Muislam au Mkristo?”
Mwandishi alipomjibu kuwa ni Muislam, akaendelea: “Sasa kipi cha ajabu
hapo? Kwa imani yake ya Kiislam, ana ruhusa ya kuoa wake hadi wanne.
Halafu kuna wakati nilishaishi naye miaka si chini ya minne, kwa hiyo
sioni ajabu hapo. Hata kama ikitokea tena hakuna tatizo"
Batuli aliyejaaliwa mvuto wa haja alimalizia kwa kusema "Achana na watu bwana, acha tu watu waongee. Lakini ninachosema hakuna cha ajabu hapo. Maisha yanaruhusu, yaani kisheria hata Mungu anaruhusu - siyo ajabu. Siwezi kuzungumza zaidi maana nimesafiri nipo kwenye harusi, dada yangu anaolewa"
Batuli
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni