DIAMOND NI NOMAAAA BABAAKE, ANGALIA 'NUMBER 1 RMX YA DIAMOND ILIVYOMPA SHAVU NCHINI UFARANSA
Kwenye
Top 10 ya muziki mkali wa Afrika ambayo hufanyika kila Alhamisi kwenye
kituo cha TV cha Ufaransa ambacho kina mamilioni ya Watazamaji Afrika
(TRACE TV Urban) May 1 2014 single ya ‘number one rmx’ Diamond ft Davido
imeshika nafasi ya nne.
Kwa
zaidi ya wiki sita hii single imekuepo kwenye chati hizi za Trace Urban
ambapo ilishika namba 1 kwa zaidi ya wiki mbili kwenye kituo hikohiko
toka iachiwe rasmi January 6 2014.
Kwenye
hiyo chati wiki hii number tatu imeshikwa na single ya 2Face ft T Pain,
ya pili Aye ya Davido na ya kwanza ni ‘rands and nairas’ ya Emmy Gee ft
Ab Crazy & Dj Dimplez.
Diamond
amevunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki kuingia
kwenye chati hiyo na kushika nafasi ya kwanza ambapo kabla ilikua
imezoeleka ni Wanigeria na Wasouth Afrika ndio wanaoongoza kwa
kuishikilia.
Kwenye Exclusive interview na mtandao mmoja nchini Kenya Diamond
alisema kingine alichogundua kwenye hii single ni ukubwa ilionao nchini
Ghana kuliko hata Nigeria kwenyewe kwa kina Davido.
Mpaka
sasa ‘number 1 rmx’ kwenye Youtube imetazamwa kwa zaidi ya mara milioni
1 na laki sita ambapo mpaka saa kumi alfajiri ya May 2 2014 ni watu
4991 walikua wameipenda kwa kulike huku 546 wakidislike.
Number
1 original ya Diamond ambayo iliwekwa kwenye mtandao September 2 2013
imetazamwa zaidi ya mara milioni mbili laki mbili na elfu 95 ambapo 5165
wamelike huku 618 wakidislike.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni