HIKI NDIO CHANZO CHA KIFO CHA MWIGIZAJI WA BONGO MOVIE ADAM KUAMBIANA
 |
Adam Kuambiana |
Habari zilizoifikia Swahiliworldplanet muda
huu ni kuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini ambaye pia ni director
Adam Kuambiana Amefariki dunia muda mchache uliopita baada ya kuanguka
ghafla akiwa location. Chanzo makini ambacho pia ni star mkubwa wa
filamu nchini kimeitumia ujumbe SWP uliosomeka "msanii Adam Kuambiana
amefariki dunia sasa hivi, alikuwa location kaanguka ghafla, maiti ipo
hospital ya Marie Stopas, Mwenge, Dar es salaam. Mungu ailaze roho yake
mahali pema peponi. Ameen.
Enzi za uhai wake Kuambiana alianza kujipatia umaarufu baada ya kuigiza
filamu ya Fake Pastors na baada ya hapo kucheza filamu nyingi zilizompa
umaarufu kabala ya kuanza kuwa director.
Tutawaletea updates zaidi kuhusu kifo cha Kuambiana ambacho ni pigo katika tasnia ya filamu nchini.
Adam Kuambiana
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni