ROSE NDAUKA ATWAA TUZO YA BEST ACTRESS 2013/2014 ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL
 |
Rose Ndauka |
Star mwenye jina kubwa na kipaji cha kuigiza Rose Ndauka ameshinda tuzo
ya muigizaji bora wa kike 2013-14(Best actress of the year 2013-2014)
kutoka Zanzibar International Film Festival 2014 ambalo ni tamasha la
filamu la kimataifa linalojumuisha watengeza filamu na wasanii
mbalimbali kutoka nchi mbalimbali. Rose ameshinda tuzo hiyo kutoka
kwenye category ya muigizaji bora wa filamu za Tanzania kupitia filamu
ya
Waiting Soul ambayo alicheza na star mwenzake Mohamed Mwikongi "Frank" . Jamila Jailawi na Yasinta Enrendry.
Swahiliworldplanet
ilipomuuliza mwigizaji huyo mwenye mvuto wa asili amejisikiaje baada ya
kutwaa tuzo hiyo Rose alisema "nimejiskia furaha sana, pia imekua
zawadi yangu kubwa hamuwezi amini.. kwa kutoweza kutoa filamu kwa muda
mrefu ila nimeweza kuwapatia nilichokipata baada ya kuvuna mashabiki
wangu...
niko na furaha na nawashukuru wote, namshukuru mama yangu
mzazi na ndugu zangu.. pia namshukuru Director wangu kwenye filamu hii
Malick Bandawe na pia napenda kuishukuru NDAUKA ENTERTAINMENT kwa
ujumla.....NAWAPENDA ZANA NA NAWASHUKURU WOTE KWA KUWEZESHA KAZI YANGU
KWA NAMNA MOJA AMA NYENGINE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni