Kwa mara ya kwanza kwama UHARIRI WA DOMOZEGE najitokeza kuuliza
swali ambalo nahisi majibu ninaweza kuwanayo ila labda sijajua kuwa haya
nilionayo ndio majibu sahihi..(Siunakumbuka enzi za soma hadithi hii
kisha jimu maswali hapo chini....). Leo hii nataka kukuja hivi huyu Wema
Sepetu ni nani? kwamaana kuwa anafanyanini hapa nchini hadi kuwa mtu
maarufu kihivyooooo na hadi kuwa na mashabiki ambao wameapa kumpenda na
kusapoti kila anachokifanya hata kama ni Negative (mara nyingi huwa -)......Mbali ya wale
wanamfuatilia kupitia magazeti ya UDAKU (uswazi ndio wengi hawa)..kwenye mitandao ya kijamii kama
FESIBUKU, TWITA na INSTAGRAMU kuna vikundi na watu mmoja mmoja wanao
simama upande wawema kwamajiana tofauti tofauti...Kwapamoja wanajiita
TEAM WEMA (Naamini wanaisoma hii)
Kwakifupi
mimi binafsi nilimsikia Wema Sepetu kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2006
akiwa mshindi wa taji la MISS TANZANIA 2006....(Kama unakumbuka ushindi
wake uliandamwa na kashfa za rushwa za ngono, na fitina kibao)..Baada ya hapo hakufanya
vizuri kwenye mashindaono ya MISS WORLD ya mwaka huo akiwa kama mshiriki
kutoka TANZANIA. (Enzi hizo nahisi Diamond alikuwa hana hata Simu ya mkononi)
Baada
ya hapo zikafuata kashfa mbalimbali za Ku-DATE na mstaa Kadhaa kuanzia
wa muziki, maigizo, Madingi nk (List ya majina ni ndefu sana itatujazia
page)
Miaka
ya hivi karibuni akaibukia Bongo Movie na kuwa muigizaji, na kacheza
filamu kadhaa (Enzi za kila demu mzuri au miss anaingia kwenye tasnia).
Enzi ya ZE GRETI KANUMBA (R I P, bro wewe ndio MUINZIGA HUKU)....Kama
kawa huku nako alifanya vizuri kidogo (kibongo bongo)
FOMEKINGI LONGI STORY SHOTI
Hatimaye akatua kwenye mikono ya Diamond baada ya kuwa na mastaa kadhaa (Daah hapa kuna ka -list tena kabla ya Diamond)
Kwasasa
ni C E O wa kampuni yake ya ENDLESS FAME (kua yake au sio yake hapa sio
Ishu) inayojishughulisha ya maswala ya MOVIES PRODUCTION,
NK..Ambayo aliifungua siku za hivi karibuni. Mwisho kabisa nimeambiwa
anakipindi kwenye TV, sijajua kinaitwaje BUT nasikia anajizungumzia
mwenyewe na maisha yake....akiwa na wale jamaa zake (and of coz bila
kumsahau Meneja wake......hehehehe)
And business as usually, Kila siku yupo kwenye Media na skendo
tofauti tofauti mara kagombana na huyu kisa BWANA, mara Ndugu wa Diamond
hawamtaki...basi ilimladi watu wamsikie tu (Diamond alishaeleza mara
kadhaa kuwa Wema huwa anazipeleka mwenyewe skendo kwa magazeti ya
UDAKU-Nanasikia mwaka huu wamempa na TUZO).
Sasa kwanini nimeuliza:
Kwanza kabisa ni kweli Story za Wema ndio zinazoongoza kwa kusomwa na
wapenda Udaku watu wa Blogu (Kama mimi), Magazeti ya Udaku, majarida na
Radio,TV watakubaliana namimi kuwa story za huyu MDADA siauza sana
(Kwahiyo zinapendwa)
Kwenye mitandao ya kijamii Wema Sepetu ana watuwengi zaidi wanao
mfuatilia kuzidi mastaa wote wa hapa BONGO: Tuanze na FESIBUKU ana
LIKES zaidi ya LAKI MOJA, TWITA na Followers zaidi ya ELFU THEMANINI,
INSTAGRAM ana Followers zaidi ya LAKI NA ISHILINI...Hatari Sana...hakuna
staa yoyote anamkaribia kwanye hili.
Akounti za TEAM Wema nazo zina watu wakutosha (Kazi yao kubwa ni kusifia na kusafisha hali ya hewa kama Wema amaichafua)
Kwamfano ipo hii inajiita WEMA REPLIES wapo INSTAGRAM (Hawa kutwa wao wema tu)
Sasa facts zipo hivi:
Kwenye U-MISS; Hivi Wema anamfikia kweli Nancy Sumari ambaye alitwaa taji la Afrika?Kwenye Kuigiza; Hivi Wema anauwezo gani wakumzidi Johari au Monalisa?
Kwenye TV: Hivi kipindichake kina ubunifu na mvuto gani? unawza kufananisha na kipindi kama wanawake LIVE,au Mkasi?
Nikweli kwamba Wema hana chakumfanya awe hivi alivyo....Naomba wadau mnisaidie kuniambia
HUYU WEMA NI NANI KUWA USHAWISHI KIASI HIKI?......
Ni mtazamo tu!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni