MAMBO YAZIDI KUMUWIA MAGUMU KAJALA, SASA AAMUA KUIKIMBIA BONGO.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko wikiendi iliyopita, mwigizaji huyo
alisema anapenda awe na maisha ya furaha na wanawake wenziye kwa
kubadilishana mawazo ya hapa na pale lakini kwa sasa hana upendo huo kwa
kuwa kuna watu wanaishi kwa kutegemea bifu.
“Unajua inauma sana, unaenda klabu unamkuta mtu ambaye huko nyuma
alikuwa shoga’ko, kula, kuvaa na kila aina ya ushirikiano mnapeana, sasa
mnakuja kugombana, kiukweli roho huwa inauma ndiyo maana nashindwa hata
kwenda klabu kuepusha mengi, nasubiria viza yangu itoke nisepe zangu
China,” alisema Kajala.
Kwa muda mrefu kumekuwa na ugomvi usiokwisha kati ya Kajala na mwigizaji mwenzake, Wema Sepetu.
Kwa muda mrefu kumekuwa na ugomvi usiokwisha kati ya Kajala na mwigizaji mwenzake, Wema Sepetu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni