vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Jumapili, 15 Juni 2014

  video ya diamond kutoka leo juma  tatu!!!!!

              
Baada ya Diamond Platnumz jana (June 12) kuachia rasmi single mpya ‘Mdogomdogo’ ambayo ni kwaajili ya soko la nyumbani Tanzania, ametangaza ujio wa video ya wimbo wake mpya wa kimataifa aliomshirikisha staa wa Nigeria, Iyanya.

                   

Ingawa kuna baadhi ya watu wamebahatika kuiona video hiyo kupitia Channel O, lakini Platnumz amesema alikipatia kituo hicho video mapema lakini hakuwa amewaruhusu waanze kuicheza, na sasa itaanza kuchezwa rasmi katika vituo vya kimataifa Jumatatu ijayo.

“Kwahiyo Jumatatu tunaanza kuiachia kule kwingine”, amesema Diamond kwenye kipindi cha Power Jams kupitia EA Radio jana.

Hivi karibuni Diamond alitangaza kutoa nyimbo mbili kwaajili ya masoko mawili tofauti, la hapa nyumbani na soko la nje.

“Unajua nimeplan kuachia wimbo wa kimataifa na asili ya kutoka nyumbani na sababu ya kufanya hivyo Watanzania tulivyo ukitengeneza wmbo wa International yenye asilimia 50 ya vizungu, usifikiri kila mtu ataipenda. So na mimi market target yangu ilikuwa sehemu nyingine kwasababu nafanya hii kazi nyumbani lakini nataka soko la nje.” Amesema Dimond.

“So ili kutoa hilo swala lisilete matatizo mi nimeamua kuifumua kule so atakayeiona yeye shabiki kama hii ngoma kali inastahili kuja basi ataipa…kama atakayeiona si ya kwake ataiacha iende kule kule ataskia tu mi nashow Benin[…]kwasababu Tanzania tulivyo tunapenda vya kwetu, mi nafurahi kuwa hivyo na ndio maana naamua nitoe cha kwetu, mi nafurahi kuwa hivyo na ndio maana naamua nitoe cha kwetu na nitoe cha kule[…]kwasababu ngoma za kutoka nyumbani nyimbo tunazoimba sisi ukitaka soko la East Afrika ushike vizuri ni ngumu sana kupenya kule.”

Video ya wimbo wa Diamond na Iyanya imefanyika London, Uingereza na imefanywa na muongozaji Mnigeria aishiye UK Mr Moe Musa, aliyeongoza video za mastaa wengi wa Afrika kama Wizkid, Tiwa Savage na mpya ya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni