vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Alhamisi, 31 Julai 2014


GARI LA MSANII WA BONGO MOVIES
 
 DUDE LAKAMATWA KWA UJAMBAZI



GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, gari hilo aina ya Vitz lenye namba za usajili T 360 BAJ, lilikutwa likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya Seif Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za usajili T 296 CSC iliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.

Inadawa kuwa muda mfupi baada ya kukamatwa, Dude alitokea Polisi na kulitambua gari lake, lakini maelezo yake hayakuwatosheleza Polisi hivyo kumshikilia katika kituo kidogo cha Polisi Mabatini hadi kesho yake alipodhaminiwa.   

Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Dude ili azungumzie taarifa hizo, lakini aliwataka kufuatilia jambo hilo katika kituo cha Polisi, akisema suala hilo lipo mikononi mwao.

Shauri linalomkabili msanii huyo limefunguliwa kwa Jalada namba .KJL/RB/6399/14 UNYANG’ANYI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni