vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Jumanne, 5 Agosti 2014

Baada ya Ay kufika kwa Obama

Zamani kwenye sehemu kubwa ya wazazi kwenye familia za kiafrika walikua hawapendi wala kutaka kusikia kwamba watoto wao wanapenda usanii au kufanya muziki ila kwa sasa taratibu wanaanza kuelewa na kubadilika kwa wakati.

Mafanikio ya kimaisha wanayoyapata mastaa wa muziki ambao hawajatoka nje ya mstari wa maadili pamoja na kwamba wamefanikiwa au kupata umaarufu, yanaweza kuwa somo kabisa kwa kila alieudharau au kuuchukulia poa muziki.

Staa wa single ya Asante ambayo ipo kwenye nafasi ya 3 kwenye Clouds FM Top 20, Ambwene Yessaya ni miongoni mwa mastaa wachache wa Afrika ambao wamepewa mwaliko wa kukutana na Rais Barack Obama wa Marekani.



Ay ambae yuko Marekani na mastaa wengine wachache wa Afrika akiwemo Mkenya Victoria Kimani, D Banj, Buffalo Soldier na Femi Kuti, kwa pamoja wanatarajia kukutana na Rais Obama, 5 August, 2014.

Ikiwa ni exclusive on DStv.com Ay ameiambia tovuti hii kwamba kwenye ikulu ya Marekani 3 August wametembelea na kuonyeshwa yakiwemo makazi ya Rais, ofisi, walitembezwa pia kwenye ule ukumbi Ikulu ambao ulitumika kutazama jinsi Osama Bin Laden alivyokamatwa.

Ay na hao mastaa wengine wa Afrika wapo kwenye project ya ONE Campaign, kampeni inayosisitiza Waafrika hasa vijana kujihusisha na kilimo ambacho wengi wanakichukulia kimzaha lakini kina maisha bora ndani yake.

Wapenda mziki zake Fela Kuti babake Femi? Tazama Felabration Saturday, 9 August at 17:35 CAT katika Vox Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni