vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Alhamisi, 21 Agosti 2014

KIMENUKA MBAYA: DIAMOND PLATINUMZ KIKAANGONI NA KAMANDA NZOWA...!FULL STORI IKO HAPA! 

NI kweli kimenuka! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yupo kikaangoni, habari zinadai kwamba kila anaponyanyua miguu, kikosi cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini chini ya kamishna wake, Godfrey Nzowa nao wananyanyua miguu yao kumfuatilia.
Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi.
Habari za kiintelijensia zilidai kwamba, kisa cha kikosi hicho kufanya hivyo kinadaiwa kuwa, serikali inamhofia kujihusisha na biashara hiyo haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ nje ya nchi kwa kutumia kivuli cha kwenda kufanya shoo.
Akizungumza na wanahabari wetu jijini Dar, Jumatatu iliyopita, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kitengo hicho ambaye hakupenda kuchorwa jina gazetini, alisema Diamond amepewa maelekezo yote muhimu. 

MAELEKEZO ALIYOPEWA
“Tumempa maelekezo Diamond, atuletee mikataba ya shoo zote anazokwenda kuzifanya nje ya nchi ili tujiridhishe kama kweli ni halali au anakwenda kwa ajili ya biashara nyingine.
“Hiyo yote inatokana na uchunguzi wetu kwake kuhusu akaunti zake za benki kuonesha kwamba ana fedha nyingi sana zinazotia shaka kama amezipata kihalali,” alisema afisa huyo.
‘Diamond Platnumz’ akiwa kazini.
KUNUNUA NYUMBA
Afisa huyo aliendelea kusema kwamba, uchunguzi wao pia umebaini kwamba, msanii huyo wa Bongo amekuwa akinunua nyumba kila anaporejea kutoka kwenye shoo zake nje ya nchi, jambo ambalo taasisi haiamini kama kweli analipwa pesa nyingi kwa shoo moja, kiasi cha kumwezesha kununua nyumba jijini Dar. 


“Tumebaini kwamba Diamond kila akirudi nchini kutoka kwenye shoo zake hununua nyumba. Analipwa kiasi gani cha fedha kule kwenye shoo? Hapa ndipo tunaposimamia sisi,” alisema afisa huyo huku akigongea msumari kuwa Diamond mwenyewe amekatazwa kuzungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu kutakiwa kuwasilisha mikataba ya shoo zake za nje. 

KUNA UKWELI?
Amani lilifuatilia na kubaini kwamba, Diamond aliporejea kutoka kwenye safari yake ya Marekani hivi karibuni, alinunua nyumba kwa Sh. milioni 80 iliyopo maeneo ya Mwananyamala-Magengeni, Dar.

Siku za nyuma, msanii huyo aliwahi kuripotiwa kununua nyumba zaidi ya mbili maeneo ya Kijitonyama, Dar, kiasi cha kuandikwa na vyombo vya habari kwamba amenunua mtaa.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa.
KUHUSU AKAUNTI YA BENKI
Diamond mwenyewe aliwahi kuhojiwa katika Kipindi cha Take-One kinachorushwa hewani na CloudsTV ambapo alipoulizwa akaunti yake inasomaje, alijibu kuwa ina zaidi ya bilioni moja hivi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni