vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Alhamisi, 28 Agosti 2014

MAMBO HADHARANI: AUNT EZEKIEL NA MOSES UKWELI WA MAHUSIANO YAO HUU HAPA! JAMAA AFUNGUKA LIVE! 
Mcheza shoo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Moses Iyobo amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuenea uvumi wa kutoka kimapenzi na mcheza filamu mahiri Bongo, Aunt Ezekiel kuwa hawezi kumuacha msanii huyo ng’o.

Mcheza shoo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Moses Iyobo (katikati).
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Moses alisema kuwa kutokana na maneno mengi kuenea kuwa anatoka na Aunt, ameona ni bora aweke wazi hisia zake kwamba ni kweli anampenda msanii huyo na kuwa naye mbali itakuwa vigumu.
Mcheza filamu mahiri Bongo, Aunt Ezekiel.
“Mengi yameongelewa sana sasa naweka wazi kuwa nampenda sana Aunt. Unajua kama mtu haukuwa na uhusiano naye mara unaanza kusikia vitu vya ajabu bora tu ufanye kweli hata kama wanakusema wakuseme kihalali na si vitu ambavyo si vya kweli,” alisema dansa huyo ambaye ni mume wa mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Mwengi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni