DIVA NA AUNT EZEKIEL WASHIKANA MASHATI KISA UJAUZITO WA AUNT EZEKIEL
Staa
wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amemvaa prizenta wa Kipindi
cha Ala za Roho cha Redio Clouds FM, Lovennes Malinzi ‘Diva’ kwa madai
kwamba amemtangaza mitandaoni kuwa amepachikwa ujauzito na mume wa mtu
ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Peter ‘Moze Iyobo’,
jambo ambalo ni uongo.
Akizungumza
kwa masikitiko ya hali ya juu, Aunt alisema kuwa hakutegemea mtu kama
Diva angetumia nafasi yake ya utangazaji kumchafua akimsingizia kuwa ni
mjamzito, jambo ambalo limemsababishia matatizo kwenye ndoa yake na
mumewe Sunday Demonte.
“Mwanamke kuwa mjamzito si jambo baya lakini kunichafua mbele ya jamii eti nina mimba ya Moze Iyobo, imeniuma sana.
“Hebu
vuta picha wakwe, mawifi na mashemeji ambao tayari wameshasikia na
kusoma kwenye ukurasa wa Diva, akisema mimi nina mimba ya yule mtoto,
dah! Nimeumia sana, kwa kweli siwezi kuliacha lipite hivihivi.
“Huyo Diva lazima nitasimama naye mahakamani,” alisema Aunt.
Hivi karibuni, kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diva aliandika: “Wakati
sakata la mtoto mzuri Aunt Ezekiel ana mimba ya Moze Iyobo likipamba
moto, mimba ambayo ni tangu Mwezi wa Ramadhan, sasa hesabuni miezi, hapa
ni miezi miwili au mitatu.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni