MMH..SHILOLE KIUNO, BARNABA MAHABA TENA?!
WASANII waliowahi kuogelea katika dimbwi zito la mahaba kisha kumwagana, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’ na Elias Barnaba ‘Barnaba Boy’, wamezua maswali mapya kwa mashabiki na kuleta tafsiri kuwa huenda wamerudiana.
Mastaa wa Bongo Fleva Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’ na Elias Barnaba ‘Barnaba Boy’ beneti.
Tukio la wawili hao kugandana kama zamani lilijitokeza juzikati
walipokuwa kwenye shoo ya Serengeti Fiesta, Musoma ambapo kwenye gari
walikuwa wamekaa pamoja na hata mazungumzo yao yalikuwa kama ya mtu na
mtuwe. Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio alipenyezewa nyepesi juu ya ukaribu wa wawili hao, aliingia mzigoni ambapo aliwaona wako kwenye mazingira ya pamoja kila walipokuwa wakipiga misele.
Baada ya kukwepa mitego mingi ya kamera, paparazi wetu aliamua kuwauliza kama wamerudiana au laa?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni