Ommy Dimpoz: Diamond Amepotea Maboya Kwa Kushindwa Kumpetipeti Wema Sepetu na Kumtumia Ipasavyo
Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na Ommy zinasema kuwa mwanamuziki huyu amekuwa akitoa maneno matamu matamu akimsifia Wema na wakati mwingine akimnanga Diamond.
“Inawezekana kwamba wapo katika project lakini ukweli ni kwamba Wema amtawala Dimpoz akilini,mazungumzo yake yote ni kuhusu Wema na anadai kuwa Diamond amepeotea maboya kuachana Wema kwani nyota ya Wema haizuiliki hata kwa radi”, alisema rafiki huyo. Hii ni kwa mijibu wa gazeti la KIU.
Lakini kwa ujumla mahusiano baina ya wawili hawa bado yanawaweka watui njia panda kwani sio Ommy wala Wema aliejitokeza hadharani na kuthibitisha mahusiano yao, lakini mbwembewe za wapambe wao kwenye mitandao ya kijamii zionyesha kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi huku wengine wakiamini kuwa Ommy anataka kung’aa kupitia nyota ya Wema na hakuna swala la mahusiano ya kimapenzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni