TUKIO LA DIAMOND
Chanzo makini kilichoshuhudia sakata
zima kilieleza kuwa, Jumanne iliyopita Diamond aliingia kwenye ‘tifu’
zito na kijana aliyefamika kwa jina la Salehe Hafidhi ‘Ans Ken’ baada ya
kumharibia kamera yake aliyompa kwa lengo la kumfanyia kazi zake.
“Palichimbika, Diamond alimkabidhi Ans
Ken kamera yenye thamani ya shilingi Mil. 12 kama kitendea kazi maana
anafanya naye kazi. Sasa jamaa akaiharibu, Diamond alipohoji jamaa
akajibu mbovu ndipo mtiti ulipoibuka.
“Ilikuwa ni mvutano mzito Diamond
akimtaka kijana huyo amlipe kamera yake jamaa akawa analeta ubishi ndipo
Dangote (Diamond) akaona isiwe shida bora akimbilie polisi Mabatini
(Kijitonyama) kushtaki na jamaa akakamatwa na kuwekwa ndani,” kilisema
chanzo hicho.
MTUHUMIWA AKANUSHA TUKIO
Baada ya mwanahabari wetu kunasa tukio
zima, alimvutia waya mtuhumiwa (Ans Ken) ambaye aliachiwa kwa dhamana
siku moja baada ya kuswekwa lupango ambapo alikanusha kuwa tukio la yeye
kugombana na Diamond halikutokea.
“Kwanza mimi siitwi hayo majina
uliyonitajia, sina tatizo na Diamond na wala sitaki kugombana naye siku
si nyingi nimetoka naye South kufanya kazi,” alisema.
AZIDI KUJIKANYAGA
Alipohakikishiwa na mwanahabari wetu
kuwa ana RB inayomuonesha kuwa yeye ni mtuhumiwa wa Diamond, Ans Ken kwa
kujikanyaga alibadili kauli yake ya awali na kusema mtafaruku ni kitu
cha kawaida katika kazi huku pia akiendelea kukanusha.
“RB si karatasi la kawaida tu, siyo
kweli bwana. Hiyo siyo stori achana nayo, kwanza kwenye kazi kugombana
mbona ni kitu cha kawaida si kila jambo litatangazwa, hajawahi
kunifikisha polisi,” alisema kwa kujikanyaga maneno.
DIAMOND SASA
Kwa upande wake Diamond alipotafutwa simu yake iliita bila kupokelewa lakini Ijumaa Wikienda limenasa jalada la kesi hiyo aliyoifungua Diamond katika Kituo cha Poisi Kijitonyama iliyosomeka KJN/RB/2020/2016 KUHARIBU MALI.
Nay wa Mitego na gari lake lililovunjwa kioo.
TUKIO LA NAY SASA
Katika tukio jingine, Nay wa Mitego,
alinusurika kifo baada ya kuvamiwa mara mbili kwa nyakati tofauti na
watu wasiojulikana huku wakimuacha na maumivu ya kumvunjia vioo na taa
za gari zake mbili.
TUKIO LA KWANZA
Akiwa katika Mitaa ya Kinondoni
Manyanya, Februari 24, mwaka huu Nay alijikuta kwenye wakati mgumu baada
ya kuegesha gari lake aina ya Toyota Prado kandokando ya barabara
ambapo alipoingia dukani na kurejea, alikuta limevunjwa taa ya upande wa
kushoto na watu wasiojulikana.
MAJANGA ZAIDI
Kama hiyo haitoshi, usiku wa kuamkia
Februari 27, mwaka huu akiwa mitaa ya Sinza-Kamanyola, Nay alijikuta
kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana ambao
walimvunjia kioo cha nyuma cha gari yake Toyota Port aliyokuwa ametoka
nayo usiku huo na kuigesha maeneo hayo.
Akizungumzia matukio hayo, Nay alisema
hajawahi kukutana na mwaka wa misukosuko kama mwaka huu baada ya kuachia
wimbo wake wa Shika Adabu Yako ambao ndani yake ‘amewa-diss’ mastaa
kibao wa Bongo.
“Dah! Naweza kujikuta hata nikimfanyia
mtu maamuzi magumu, juzi tu nimetoka kuvunjiwa taa ya gari yangu ile
Prado, nikiwa niko kwenye hali ya kutafuta fedha ya kununua taa, leo
tena nimevamiwa na watu nisiowajua na wamenivunjia kioo cha gari yangu
hii Toyota Port.
“Najua wanaonifanyia haya ni wajinga
wachache ambao wanataka kupambana na mimi baada ya kuachia wimbo wangu
wa Shika Adabu Yako, sasa kuanzia sasa itabidi niongeze zaidi umakini
maana maadui wameongezeka japo nina RB ya kujihami,” alisema Nay.
Siku chache baada ya kuuachia Wimbo wa
Shika Adabu Yako ambao ‘uliwachana’ mastaa wenzake kisha baadaye wimbo
huo kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Nay amekuwa akipokea
vitisho mbalimbali kutoka kwa watu asiowajua licha ya kutoa taarifa
katika Kituo cha Polisi Kimara-Mwisho, jijini Dar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni