Lwitiko Adamson Mwakasala ‘Tiko’
Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI
DAR ES SALAAM:
Tumbuatumbua majipu ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ inazidi kushika
kasi nchini ambapo si serikalini tu, hata watu binafsi wako kitanzini.
Hilo limedhihirika kufuatia hivi
karibuni, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kumvamia na kumfanyia
upekuzi mkubwa wa saa saba, Lwitiko Adamson Mwakasala ‘Tiko’ au
‘Milionea Mtoto’ (pichani) wakitilia shaka utajiri mkubwa alionao.
]Moja ya Nyumba anazomiliki.
ENEO LA TUKIO
Tukio hilo lililofunga barabara ya
kutoka Sinza kwenda Magomeni lilijiri Februari 15, mwaka huu kwenye
jumba lake la ghorofa lililopo Magomeni Makuti jijini Dar jirani na
Kituo cha Daladala cha Kwa Bi Nyau.
Hekalu lake jingine
UPEKUZI KWA SAA SABA
Ilikuwa asubuhi ya saa moja ambapo
kikosi cha polisi kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay kilivamia kwenye
nyumba ya Tiko ambayo ni ghorofa mbili ikiwa na matawi matatu na kufanya
upekuzi mkubwa huku wakitaka kujua chanzo chake cha pesa mpaka kujenga
jengo hilo ambalo inasemekana linaweza kuwa hoteli, shule, hospitali au
ofisi.
“Upekuzi ulikuwa mkubwa sana. Tiko
alianza kupekuliwa saa moja asubuhi polisi wakiwa na mjumbe wa nyumba
kumi. Kazi ya upekuzi iliisha saa nane mchana,” kilisema chanzo.
Magari yake yaliyokamatwa yakiwa kituo cha polisi
POLISI WAONDOKA NA MAGARI, WASHIKILIA GHOROFA
Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya
upekuzi wao, polisi walimchukua Tiko na magari yake manane kwa ajili ya
uchunguzi pia wanalishikilia ghorofa hilo huku uchunguzi zaidi wa kujua
anapataje pesa ukiendelea.
NI MATAJIRI WATATU
Ndani ya wiki moja sasa, inasemekana
watu wengine wawili wenye fedha zao wamekamatwa akiwemo aliyejulikana
kwa jina moja la Hemed, mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar na mwingine
mkazi wa Tabata ambaye jina lake halikupatikana mara moja. Wanashikiliwa
na magari yao kituoni hapo kwa uchunguzi zaidi.
WANACHOFANYA POLISI KWA SASA
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya
jeshi hilo, siku hizi polisi wanamfuata tajiri mmojammoja na kumfanyia
upekuzi. Kama atakutwa na madawa ya kulevya, kesi anayo, akikutwa na
mali ambazo asili yake au upatikanaje wa fedha haujulikani, pia kesi
anayo.
UWAZI ENEO LA TUKIO
Kama ilivyo ada, baada ya kupata taarifa
hizo, Uwazi lilifika eneo la tukio na kufanya mahojiano na Mjumbe wa
Shina Namba 23, Muharami Daudi ambaye alikuwepo katika zoezi la upekuzi
nyumbani kwa Tiko.
“Nakumbuka ilikuwa Jumatatu, saa moja
asubuhi, polisi walifika nyumbani kwangu, wakajitambulisha kuwa wametoka
Kituo cha Polisi Oysterbay. Wakanitaka nifuatane nao mpaka kwa Lwitiko
katika zoezi la upekuzi wa madawa ya kulevya kwamba wana wasiwasi naye
katika biashara hiyo.
“Tulikwenda kufanya upekuzi kwa pamoja,
lakini hatukupata madawa ya kulevya hivyo polisi waliamua kuondoka na
magari yake manane yaliyokuwa pale na bastola kwa uchunguzi zaidi,”
alisema mjumbe huyo.
KAMANDA WA POLISI KINONDONI
ACP Christopher Fuime ni Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kinondoni. Katika mahojiano na gazeti hili, alikiri
kukamatwa kwa Tiko na watu hao wengine.
“Bado tunawashikilia Lwitiko na Hemed kwa uchunguzi zaidi na kutafuta mtandao wao.
”Unajua kunahitaji uchunguzi wa kina
ikiwa ni pamoja na kuchunguza mali zao jinsi walivyozipata kama vile
nyumba. Baadhi ya magari yao tunayo hapa tunayashikilia, tunayafanyia
kazi,” alisema kamanda huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni