Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (47) na wenzake
watatu leo wataendelea kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa Serikali Joseph Maugo alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey
Mwambapa kuwa kesi ilipangwa jana kwa ajili ya utetezi na wapo tayari.
Wakili mwingine wa Serikali katika shauri hilo ni Shadrack Kimaro.
Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala na Faraja Mangula ambao
wote walikuwapo mahakamani jana lakini Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha
anayeisikiliza kesi hiyo hakuwapo.
Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi.
Katika kesi hiyo, Gwajima anakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi anazomiliki kihalali katika usalama.
Washtakiwa wenzake George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze (39) na
Georgey Milulu wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki
bastola aina ya Berretta na risasi 20 kinyume na sheria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni