Waziri wa Katiba na Sheria amewasilisha maombi ya kuwasafirisha
washitakiwa watatu akiwemo Ally Hatibu Hassan maarufu kama Shkuba
kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kujibu tuhuma za kusafirishaji dawa
za kulevya.
Washitakiwa wengine ambao wanaungana na Shkuba ni Idd Mafuru na Lwitiko Emmanuel Adam.
Maombi hayo yamewasilishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini
ya kifungu namba 5 (1) cha Sheria ya Usafirishaji wahalifu sura ya 368
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Katika maombi hayo upande wa waziri kupitia DPP wanaiomba mahakama hiyo
isikilize ushahidi na itoe amri ya kuwahifadhi washitakiwa ndani wakiwa
wanasubiri kibali cha Waziri huyo cha kuwasafirisha nje ya nchi kwa
mashitaka hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni