Kama muelewavyo story za kuteka na kutaka kutekwa zimepamba moto na kila mtu hasa wabunge wanasema wanataka kutekwa.
janakwenye kipindi cha DW alitafutwa mbunge Zitto kuzungumzia hili swala
kwanza aliulizwa kama ana taarifa ya bashe kusema kuna wabunge 11
wanatafutwa kutekwa akasema hana taarifa kamili na ni vigumu yeye
kulielezea na alisema kuwa yeye binafsi alitonywa kuwa kuna watu saba
nje ya bunge, wabunge na mawaziri watatu wanapangwa kutekwa....
Lakini Zitto aliulizwa una uhakika gani na vyanzo vyako kama
havikudanganyi? alisema yeye ametonywa na ana haki ya kuchukua
tahadhari.. hata hivyo aliulizwa mbona taarifa zake na mbunge wa Nzega
zinakindhana mwenzie anasema watu 11 na yeye anasema watu 7 wakiwemo
mawaziri? Zitto alijibu kwa kusema yeye hajui vyanzo vya bashe vilivyo
mpa taarifa ila yeye ana vyanzo vyake hivyo siwezi jua vyanzo vya Mh
Bashe.
Pia Mh Zitto aliulizwa kama anamjua muhusika wa utekaji huu akasema
angekuwa anamjua asingelipiga kelele na wala isingekuwa mjadala tena...
Pia Mh Zitto alisema kuwa yeye kesho atawasilisha hoja bungeni kutaka
waunde kamati maalum ya kuchunguza matukio hayo ya utekaji na lazima
watu wawajibike
Source: DW(6:00-6:30 PM)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni