vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Jumanne, 26 Julai 2016

Raymond: ‘Natafuta Kiki’ inakwamishwa na wasanii niliowataja katika wimbo


Msanii wa muziki kutoka WCB, Raymond aka RayVanny ameitaja sababu kubwa ya kuchelewa kwa video ya wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ kuwa ni baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo huo kushindwa kuonesha ushirikiano.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV kuwa baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ wamekuwa wagumu kupatikana.

Aidha Raymond ameongeza kuwa menejimenti yake ilimleta director kutoka nje lakini baada ya baadhi ya wasanii kushindwa kuonesha ushirikiano wakamruhusu kurudi kwao kwanza.

Kutokana na mashabiki wengi kuwa na hamu ya kuiona video ya wimbo huo, Raymond ameachia video ya wimbo huo ikiwa ni Guitar Version. Hata hivyo Raymond amedai video hiyo itafanyika japo hajataja itachukuwa muda gani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni