Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amedai wanaomuita shujaa leo ipo siku
wanaweza kumgeuka kwa sababu kama binadamu bado ana safari ndefu na
anaweza kujikwaa ndiyo maana hataki kulivaa jina hilo bali anahitaji
watanzania waendelee kumuombea.
Akizugumza akiwa Mtama Mh. Nnauye amesema hawezi livaa jina hilo bali
amelipokea kwakuwa wananchi wameamua kumpatia jina hilo kwani hata
sababu za kuitwa jina hilo zipo tofauti tofauti.
"Sikatai kuitwa Shujaa kwa sababu wao wenyewe ndiyo wameniita, lakini
siyo jambo ambalo nitalivaa. Hao hao wanaoniita shujaa siku nyingine
wanaweza kunigeuka kwa sababu binadamu ukiwa hai unaweza kujikwaa safari
bado ni ndefu nachotaka kuwaomba tu wananchi waendelee kuniombea. Hata
hivyo sababu za kuitwa shujaa kila mtu ana sababu yake, mwingine
atakuambia kwa sababu hujatetereka wengine wanasema umesimamia ukweli,
kwa hiyo jina hilo siwezi kulivaa ila siwezi kulikataa". Alisema Nape
Mh. Nnauye jana alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Mtama kwa
mara ya kwanza baada ya kuvuliwa uwaziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo Machi 22 mwaka huu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni