vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Jumatatu, 10 Aprili 2017

Simulizi..Jinsi Roma Alivyotekwa From A- z..!!!


Kaka wa Roma Mkatoliki, msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyetekwa akiwa na wenzake na kurejeshwa juzi, amesema watekaji waliwafunga vitambaa vyeusi usoni, lakini hadi sasa hawawajui wahusika na waliwarejesha na kuwaacha Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
Pia, kaka huyo, Omari Musa amesema Roma, ambaye alipata umaarufu kwa nyimbo zake za kukosoa ukandamizaji wa vyama vya upinzani hasa katika wimbo wa “Viva Roma”, hakuwa anarekodi wimbo mpya kama inavyodhaniwa.
Licha ya polisi kukana kuwa watu hao hawakuwa wanashikiliwa katika kituo chochote cha polisi, Roma na wenzake walionekana Kituo cha Polisi Oyesterbay, Kinondoni ambako walihojiwa kwa zaidi ya saa sita baadaye kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala.
Baada ya kutoka, Roma alizungumza kwa kifupi akiwashukuru Watanzania na kusema atazungumza na wanahabari leo. Lakini, Musa alisema Roma hayupo tayari kuzungumza mambo mengi yaliyompata au alichofanyiwa na watekaji hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni