Anaeongea kwa sasa ni msanii Roma na anatoa shukrani kwa wote bila
kujali itikadi zao, anasema kilichowapata watu wafanye kama case study.
Roma anasema hawana uhakika wa usalama wao hata kidogo, amesema nature
ya tukio, studio zilizopo Tongwe records yuko tangu 2007 na ni eneo
salama sana. Amesema wana majirani wanaowapa amani sana ikiwemo ujirani
na Tibaigana, Waitara na mstaafu mmoja wa Magereza.
Amesema hofu hiyo isiishie kwao kwani inaweza ikarudi kwa yeyote muda
wowote, mtu yeyote inaweza kumkuta. Amedai wao ni wachanga mno na
hawawezi kupambana na yeyote. Anasema Bin Laden hayuko sawa na anastuka
sana mpaka kuwastua watu wote.
Amedai kuna watu wanaamini hakuna kilichotokea kwa kudhani ni kiki na
wengine wanasema wanatumika kisiasa labda kuchafua serikali.
ROMA: Tunatafuta ruzuku yetu kupitia mziki, tumelia sana kwa haya maneno
tena mengine kutoka kwa watu wa karibu sana ikiwemo wanamuziki, si
kweli. Tunaishi familia za kawaida na hatuwezi kurisk maisha yetu kwa
ajili ya hela au sababu nyingine yeyote.
Kilichotokea ni kweli, nadhani mnaona mwili wangu(anaonyesha),
linatuumiza sana mtu kusema tumepewa dola 5,000. Tumeumia, tumepigwa
kiukweli na tumeripoti kwenye vyombo vya dola.
Sheria zetu zinasema jambo likianza uchunguzi ni njema kulielezea kwani wanasema linaharibu upelelezi.
Nilifika Tongwe na kuwakuta wenzangu, haikupita nusu saa wakaja watu na
silaha za moto na amri ilikuwa kuingia ndani ya gari, tukiwa tumefungwa
usoni na pingu, ilikuwa Jumatano jioni na tumekuja kupata usalama
tumekuja kuupata Ijumaa jioni na kulikuwa na mahojiano yanaendelea
yakiambatana na vipigo. Maojiano hayo ndo hayo temsharipoti.
Tulifungwa tena na kuachwa eneo ambalo hatulijui tukatupwa kwenye dimbwi
la maji, tukajikuta tuko salama na baada ya kutembea sana tukakuta
kibao kimeandikwa Mahaba beach na kugundua tulikuwa Ununio.
Swali: Mlingundua mlitupwa beach, mlienda beach Oysterbay police
JIBU: Ilikuwa ni usiku, baada ya muda tulipogundua Ununio, nilikuwa na
madoa ya damu. Mpaka mtu ujue mimi ni Roma ilikuwa ngumu, tulifika hadi
Kunduchi na kukuta boda sita na kumuomba Moni aite boda, tukaenda hadi
nyumbani Mbezi, kuingia ndani hamna mtu, nikawaambia wenzangu tubadili
nguo, ilikuwa inaelekea Alfajiri, mtu wa bajaji tukamuomba simu kumpigia
bosi wetu.
Tulipofika alikuwa tayari amempigia Ruge Mutahaba, walikuwepo na
waliumia sana, wao ndio wakatupa way forward na kusema walifungua hii
kesi kituo cha polisi hivyo tukaenda kituo cha polisi Oysterbay.
SWALI: Waliwaachia masharti yoyote
JIBU: Ipo ndani ya upelelezi.
SWALI:Chanzo kilikuwa mziki wako?
JIBU: Siwezi kujua, upelelezi unaweza kuleta majibu.
Dada anaeonekana muongozaji anasema hamna swali jingine na anamkaribisha waziri Mwakyembe.
Mwakyembe: Pale ambapo kuna tatizo na msanii yeyote nitaarifiwe kwanza
mimi waziri mwenye dhamana, wasanii wote ukihojiwa na mtu usiemjua wa
ajabu nitafute, niliposikia taarifa hii nikajiuliza chombo cha dola
kimekiuka tena taarifa yangu? Hili ni swala scientific tuache kupiga
ramli, wenzetu wamesema tuwaache wafanye upelelezi, hii sio hali ya
kawaida
Inaweza kuwepo wasanii(sio wanamuziki) wachache wanataka kutuvuruga, nawashukuru sana.
SWALI: Bashe amesema vyombo vya usalama vimehusika
JIBU: Umeleta maswala ya kina Bashe, mimi hapa Mwakyembe, mambo hayo yako bungeni.
Swali: Kuna mtu alisema Roma ataonekana kabla ya Jumapili na kweli akaonekana
Moderator: Sasa tuishie hapohapo.
Mwakyembe: Mkiendelea kupiga kelele kama watoto wa shule naondoka hapa,
wewe unaamini ni vyombo vya dola? Siwezi kuamini mpaka nione ya
recording ya huyo kiongozi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni