JOH MAKINI NA NIKKI WA PILI NDIO WAMEAU KUNDI LA NAKO 2 NAKO NA RIVER CAMP! KAMA HUJUI BASI SOMA HAPA
Mara nyingi Nikki wa Pili kama msemaji wa kundi la WEUSI amekuwa
akinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akidai kwamba weusi si kundi
bali ni kampuni ambayo haina uhusiano wowote na kundi la rivercamp
soldiers ambalo lilikuwa linaundwa na Joh Makin, Nikki wa Pili, Bonta na
wengineo na pia haliingiliani na kundi la Nako2Nako lilikuwa likiundwa
na Gnako&Lord eyez na waliojitoa mapema Bu Nako na Ibra da.
Nikki anasema kuwa kuwa makundi ya rivercamp soldier na Nako2Nako
hayajafa na bado yanaendelea na shughuli zao, ukweli ni kwamba makundi
haya wawili yalishakufa tangu tu pale kundi la weusi lilipoundwa. Toka
kundi la weusi limeundwa lini tumesikia kazi ya nako2nako? lini
tumesikia kazi ya rivercamp soldier kundi ambalo lilikuwa lipolipo tu
halina mbele wala nyuma.
Joh makini na Nikki wa Pili ndio wameyaua haya makundi kwasababu za
kimaslahi, kwanini Bonta hayupo kwenye kundi la WEUSI? Walitumia vigezo
gani kuunda hiyo kampuni?
Kama wao walihisi wakifanya nyimbo kati ya John Makini, Nikki, G nako na
Lord Eyez ndio inakuwa nzuri basi ni vema wakawa wawazi kuwa washajitoa
kwenye makkundi yao na waunda kundi jipya kuliko kuwadanganya wenzao na
watanzania kwa ujumla.
Kulikuwa kuna umuhimu gani wa kuunda hiyo kampuni ya weusi wakati kundi
lenu tu la rivercamp soldiers halijafanya chochote kinachoonekana kwa
jamii? Kulikuwa na umuhimu gani wa kuunda kampuni ya weusi wakati kundi
la nako2nako lilikuwa bado halijasimama vizuri? ni kipi hasa mlichokuwa
mkikitafuta ambacho hakipo kwenye makundi yenu?
MCHAWI WA MSANII, NI MSANII MWENYEWE. OVER
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni