MSANII RACHEL HAULE WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA!
Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki
dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini
Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti
wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili
jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye
hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa
mbaya na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa
msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo
hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo.
Habari na picha zaidi zitawajia baadae.
Credit:GPL
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni