vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Jumatatu, 14 Julai 2014

MMH..FASHENI HIZI JAMANI MAJANGA…KIVAZI CHA JAQUELINE WOLPER CHAZUA GUMZO…! TWENZETU UJIONEE…

Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe
MH! Kigauni kifupi alichotinga staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kimeibua minong’ono watu kuhoji kulikoni akivae hivyo ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tukio hilo lilowastaajabisha wengi lilijiri wikiendi iliyopita katika Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki, Dar ambapo asilimia kubwa ya waalikwa katika hafla hiyo walisema hakikustaili hasa
kwenye mwezi huu wa toba. “Unajua siku zote tunaambiwa sisi Bongo Movie hatuna heshima, siyo kweli, kuna watu wapo kwa ajili ya kutudhalilisha. Angalia Wolper alichovaa,” alisema mwigizaji mmoja ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini. Alipoulizwa Wolper kuhusiana na madai hayo ya udhalilishaji, alijibu: “Achana nao hao ni wanafiki tu kwani kuna mtu amekatazwa kuvaa kama hivi?”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni