TAZAMA PICHA FUMANIZI LA HATARI,MKE AVUNGA KUSAFIRI,MUME AVUTA KIFAA NDANI,MAJIRANI WAPIGA CHABO
KUNA matukio
ambayo kama binadamu yasikie kwa wengine tu lakini yasikutokee wewe!
Kama hili la mkazi wa Ukonga –Mzambarauni, Dar, Paulo Ndulu ambapo
mkesha wa kuamkia Sikukuu ya Sabasaba, alijikuta katika wakati mgumu
pale alipoingia kibaruani kuamua ngumi kati ya mkewe, Anitha Mapunda na
Elizabeth Chacha aliyedaiwa kuwa ni hawara yake, OFM walishuhudia.
Bw.
Paulo Ndulu akijaribu kuamua ugomvi kati ya mkewe, Anitha Mapunda na
Elizabeth Chacha (mwenye shati nyekundu) anayedaiwa kuwa ni hawara yake.
OFM
ni kikosi cha kifichua maovu cha Global Publishers ambacho katika
kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kimekuwa
kikizunguka usiku ili kuhakikisha hakuna watu wanaokwenda kinyume na
swaumu za Waislam.
...Iilikuwa ni soo la kufa mtu.
OFM MITAANI USIKU
Siku ya tukio, majira ya saa nane usiku, OFM ilikuwa ikikatiza maeno ya
Ukonga jijini Dar na kubahatika kushuhudia timbwili zito sana kutoka
kwenye nyumba ya Ndulu huku majirani kibao wakiziba mtaa kushuhudia.
Bw. Paulo Ndulu akiendelea kuamua ugomvi huo.
OFM
ilisogea kwenye sekeseke hilo na kugundua kuwa, ndani ya nyumba ya
Ndulu kulikuwa na kasheshe zito la nguo kuchanika kati ya wanawakwe
wawili ambapo majirani walisema mmoja ni mke, mwingine hawara, kisa?
...Mara majirani nao walishuhudia ugomvi uliokuwa ukiendelea kwa kupiga chabo dirishani.
MSIKIE JIRANI
“Mke
aliaga anasafiri, mume akaingiza mwanamke mwingine, sasa kumbe mke
hakusafiri kikweli, alimdanganya mumewe baada ya kujua kuna mwanamke
atakuja,” alisema jirani mmoja huku akilalamika kwamba, amepika daku
linapoa kwa sababu ya kushuhudia filamu hiyo ya bure.
Ilidaiwa kuwa, Anitha alikuwa katika wakati mgumu baada ya mumewe kuwa
na tabia ya kumwingiza mwanamke huyo ndani na kumwambia yeye akakae
mahali anywe soda au aende kwao mpaka mgeni wake atakapoondoka ndipo
arudi.
Bw. Paulo Ndulu akizidi kumsihi mkewe apunguze munkari.
ALIJIFICHA
Siku ya tukio, kwa mujibu wa mashuhuda, Anitha alipobaini ujio wa mgeni
huyo (Elizabeth) alijifanya anakwenda Kimanzichana, Kisarawe, Pwani
lakini uhalisia alikwenda kujificha nyumba ya jirani huku akiweka
wapambe wampigie chabo nyendo za mumewe kwa usiku huo kwa sababu alikuwa
amechoshwa na uonevu wa kutakiwa kwenda kukaa mahali.
Bi. Anitha Mapunda(mke wa Paul Ndulu) akiwa ni mwenye ghadhabu kubwa.
MUME ARUDI, HAWARA ATINGA
Chanzo
kilisema saa moja usiku, Ndulu alionekana akirudi nyumbani hapo. Muda
si mrefu, mrembo mweupe, mrefu alionekana akiingia nyumbani hapo na
Ndulu alitoka kumpokea.
WAPAMBE WANYAKUA VIATU VYA ELIZABETH
Jirani huyo alizidi kusema kuwa, wakati Eliza akizama ndani Ndulu,
alivua viatu na kuviacha nje ya mlango. Wapambe wakavichukua na kwenda
kumuonesha Anitha akiwa mafichoni ili kumthibitishia kuwa tayari mumewe
alikuwa na kifaa ndani.
..Hawara huyo(Elizabeth Chacha) akikalishwa chini ili wayamalize kiutu uzima.
Baada
ya kuoneshwa viatu hivyo, Anitha alichanganyikiwa na kutoka kwenda
nyumbani kwake ambapo aliingia na kusababisha varangati hilo la aina
yake lililodumu kwa karibu dakika ishirini mpaka OFM ilipotokea ambapo
pia askari wa kulida doria usiku walitinga eneo la tukio.
Bi. Elizabeth chacha akisikiliza kwa hofu uamuzi uliochukuliwa.
MJUMBE ASHIRIKISHWA
Ili kuweka sawa mambo ya kisheria, maafande hao wenye maadili ya kazi
walikwenda hadi kwa Mjumbe wa Shina Namba 29, Mama Urio ambaye
waliongozana naye mpaka kwenye eneo lenye kizaazaa.Hata hivyo, polisi na
mjume huyo walimkuta Anitha ameshamvaa mbaya wake huyo huku akimtupia
maneno yenye lawama na shutuma nzitonzito kwamba anamvunjia nyumba yake.
...Majirani walifika eneo la tukio na kushudia mkasa huo.
WATU DIRISHANI WEWEEE!
Ndulu mbali ya kuchoka hoi kufuatia kazi nzito na kumdhibiti mkewe
asiendelee kuzichapa na Eliza, pia alikuwa na kazi nyingine ya kugombana
na majirani ‘wambeya’ walijaa dirishani kwa nje wakimporomoshea maneno
yenye kuudhi.
UTETEZI WA NDULU
Baada ya hali ya hewa kutulia, polisi walimuhoji Ndulu kuhusu sakata
hilo, alikiri kuishi na Anitha kwa zaidi ya miaka minne lakini alimkana
kuwa si mkewe kwa kuwa yeye ni Mkristo wa madhehebu ya Katoliki na
hakuwahi kufunga naye ndoa.
Bw. Paulo Ndulu akijaribu kuwafukuza mashuhuda wa tukio hilo la aibu.
Hata
hivyo, utetezi huo wa Ndulu ulipingwa vikali na mjumbe wa nyumba kumi
na polisi ambapo walimwambia kisheria mwanaume na mwanamke wakiishi
ndani ya nyumba kwa muda huo tayari ni mkewe.
Wakasema kwa hiyo kitendo cha kumpelekea mwanamke mwingine ndani ni kutafuta machafuko kwa makusudi.
Bw. Paulo Ndulu akijitetea kuhusu uhusiano wake na hawara huyo.
ELIZABETH SASA
Wakati wote wa sakata, Elizabeth alikuwa akipiga mayowe ya kuomba msaada
akisema amekoma kwani Ndulu alimwambia kuwa haishi na mwanamke baada ya
kuachana na Anitha muda mrefu kwa sababu za ugumba.
Bi. Elizabeth Chacha akiondoka peku peku eneo la tukio.
"Mimi
aliniambia haishi na mwanamke na nilimuuliza sana kuhusu hili naye
akanithibitishia kuwa ni msela lakini hata hivyo machale yalikuwa
yakinicheza muda wote, namuomba radhi mwanamke mwenzangu jamani,”
alisema Eliza.
MWISHO WA SAKATA
Hatima
ya sakata hilo, Elizabeth alitakiwa kurudi kwao, Ubungo -Maziwa jijini
Dar na Anitha alishauriwa kwenda kulala kwa kaka yake anayeishi jirani
na eneo hilo chini ya usimamizi wa mjumbe.
ANITHA MWENYEWE
Akizungumza na OFM baada ya kutulia kwa sekeseke, Anitha alisema miaka
minne ya maisna na Ndulu, mapenzi yalikuwa motomoto lakini siku za
karibuni mwanaume huyo alibadilika ghafla, akaamini ni baada ya kumpata
Eliza.
chanzo:gpl
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni