Katika interview mbili nimewahi kumsikia Diamond Platnumz akitoa
msemo mmoja unaofanana lakini katika hizo interview mbili tofauti, akitabasamu
alisema ‘kama nafanya kazi kwa bidii ni lazima niishi vizuri pia, nipate
ninavyotaka’
Kwa hii picha ya gari aliyopost Diamond kwenye instagram labda ndio
anaendelea kutimiza ndoto zake? japokua hakuandika chochote baada ya kuiweka
picha hii ya gari jipya lisilo na namba, baadhi ya mashabiki wameanza
kumpongeza ila bado millardayo.com inaendelea kumtafuta ili tupate uhakika kama
ndio mkoko wake mpya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni