Uongozi wa Msanii Chris Brown Upo Tayari Kufanya Kazi na Ally Kiba
Kwa taarifa zilizopo katika mtandao wa VIP Beats nchini marekani zinaeleza kua tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2014 uongozi wa msanii Chris Brown ulipokea maombi ya muungano wa wasanii wawili kufanya wimbo wa pamoja kati ya msanii Ali kiba na Chris Brown maombi hayo yaliambatanishwa na Softcopy zilizobeba nyimbo tatu za msanii Ali kiba ikiwemo SINGLE BOY,
MWANA pamoja na wimbo aliofanya katika project ya ONE 8. Uongozi wa Chris Brown umethibitisha kupokea taarifa za maombi hayo na umeonesha kupenda sauti ya msanii Ali kiba na kutoa tamko kua wapo tayari kusimamia kazi ya pamoja itakayofanywa na wasanii hawa.
Upande wa msanii Chris Brown amesema hana tatizo yupo tayari kushirikiana na msanii Ali kiba kwani alipata nafasi ya kutazama project ya One 8 na ameona kiwango cha msanii Ali kiba kinaridhisha
Japokua anahitaji marekebisho madogo sana. BBC SWAHILI Tunampongeza msanii Ali kiba kwa juhudi zake tunamtakia kila lakheri katika kazi hii, kuipata habari hii kamili tembelea mtandao wa VIP Beats, Channel 0 au unaweza kuipata katika American Spring news.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni