Wastara Awacharukia Wanao Mtukana Mumewe Mitandaoni...
Akizungumza na gazeti la Ijumaa, Wastara alisema anajisikia vibaya baadhi ya mashabiki wanavyomtukana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo siyo zuri kwani wanaingilia maisha yake binafsi na kibaya zaidi wanamhusisha Sajuki.
“Ukweli sipendi kabisa na nitamshtaki mtu maana wananitengenezea chuki kwani wakati mwingine wananitukana, wanamtukana sana Bondi huku wakidai kwamba nilikuwa naomba Sajuki afe ndiyo nifanye mabaya sasa sijui nimefanya kitu gani kibaya, kuwa na Bondi nimekuwa naye baada ya mume wangu kufariki maana mimi ni binadamu na kama angekuwepo nisingekuwa na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema Wastara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni