Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki amezungumza kwa hisia
juu ya wasanii wenzake na watu wengine ambao wanahusisha kutekwa kwao na
mchezo wa kiini macho.
“Watu wanasema tunatumika kisiasa tunataka kuichafua Serikali, wapo
wanaosema tunatafuta kiki na kuna wengine wamekwenda mbali zaidi na
kudai tumelipwa Dola 5,000 ili tutengeneze habari hii.
“Tunaumizwa sana na kauli hizo, nguvu za watu walizotumia kupaza sauti
zao halafu watu wanasema tunacheza mchezo, hatuwezi kuhatarisha maisha
yetu kwa sababu ya fedha sisi ni watu wa kawaida sana familia zetu ni
masikini, lakini hatuwezi kukubali kuumizwa hivi kwa ajili ya fedha.”
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe
amesema anataka kupata majibu ya tukio la utekaji wa Roma Mkatoliki
kabla ya kuwasilisha bajeti yake bungeni.
“Mimi nitakuwa kwa wapelelezi, nataka kujua suala hili nipate majibu
kabla sijawasilisha bajeti yangu bungeni ili bajeti yangu ipite bila
makelele mengi,” amesema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni