Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akikagua kazi ya kuondoa maji ya mafuriko kutoka katika nyumba za watu
katika eneo la Buruguruni Mnyamani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam
leo wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali
walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na kuwafariji
wananchi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimfariji mmoja wa wakazi wa Buguruni Mnyamani Bi.Halima Hamza ambaye
nyumba yake imeathiriwa vibaya na maji ya mafuriko wakati Rais na Mkewe
Mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali walipotembelea eneo hili
kujionea athari za mafuriko na kuwafariji wananchi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto Irene ambaye nyumba yao imeathiriwa na mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said
Mack Sadik akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfereji ulioziba
kutokana na uchafu na kusababisha mafuriko katika makazi ya watu eneo la
Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwahutubia wakazi wa Buguruni Mnyamani waloathiriwa na mafuriko
kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.Rais
Kikwete ameahidi kuwasaidia wananchi hao
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete
wakipita katika mitaa mbalimbali ya Buguruni leo wakati wa zoezi la
kuwafariji waathirika wa mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
(picha na Freddy Maro)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni