Leo April 12 Rais Dkt John Pombe Magufuli amezindua awamu ya kwanza ya
ujenzi wa reli ambayo itakayorahisisha usafiri wa Dar es Salaam hadi
Morogoro kwa njia ya treni.
Inawezekana mtu akawa anaishi Morogoro na kufanya kazi zake Da es Salaam
kwani usafiri utakuwa wa uhakika na haraka zaidi. Rapper Stamina ambaye
ni mzaliwa na Morogoro anayefanya mishe zake Dar, amehaidi kurudi
kuishi Moro na wakati huo huo akiendelea kufanya mishe zake Dar endapo
njia hiyo ya usafiri itaanza kufanya kazi.
“Ikikamilika hiyo Rais, naenda kuishi zangu Morogoro tu,” ameahidi
Stamina wakati akipiga story na Prince Ramalove kupitia Kings Fm Leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni