vodacom.co,tz

vodacom.co,tz

Alhamisi, 1 Februari 2018

Lulu Diva Arudisha Mwenyewe Mahali Aliyotolewa na Mchumba Wake

MWANAMUZIKI wa kike anayekuja kwa kasi Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amerejesha kwa mikono yake mwenyewe mahari aliyokuwa ametolewa na mchumba wake aliyedumu naye kwa takriban miaka mitatu.

Chanzo chetu makini kilisema kuwa, mwanamuziki huyo alikuwa afunge ndoa mwishoni mwa mwaka jana lakini kutokana na kuvuja kwa habari kuwa anatoka na mwanamuziki mwenziye wa Bongo Fleva, mwanaume huyo akadai mahari yake.

“Kama kuolewa basi Lulu angeolewa mwaka jana mwishoni lakini mchumba huyo alibaini anatoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake akaomba mahari yake irudishwe,” kilisema chanzo.
                                         Hatari Tupu!....... Lulu Diva Arudisha Mwenyewe Mahali Aliyotolewa na Mchumba Wake

Gazeti hili lilipompigia simu Lulu na kumuuliza madai hayo alisema, ni kweli alirudisha mahari lakini si kwamba mwanaume huyo alijua anatoka na mwanaume mwingine bali alipata shinikizo kutoka kwa ndugu zake.

“Aliposhinikizwa sana nikaona isiwe tabu nikamrudishia mahari yake kwa maana alikuwa akiwasikiliza sana ndugu zake ambao walikuwa hawataki anioe,” alisema Lulu.

Na Imelda Mtema

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Radio amefariki dunia.

Msanii Radio Afariki Dunia


Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel,  tangu January 23 mwaka huu hali yake ilikuwa ikiripotiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana na ugomvi wa klabu.

Hapo jana Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Milioni 30 kwa ajili ya  matibabu ya msanii huyo, pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika February 4 mwaka huu katika kanisa la Light the World.

Jumatano, 12 Aprili 2017

PICHA: Gari mpya aliyoipost Diamond leo nyumbani kwake South Africa



Staa mwimbaji Diamond Platnumz ametua South Afrika na tayari yuko nyumbani kwake pamoja na mpenzi wake Zari The Bossy Lady. Kati ya vitu amevipost Diamond leo kupitia Instagram yake leo ni pamoja na picha ya gari jipya ambalo kwa mujibu wa maelezo yake amelinunua kwaajili ya kupigia misele atakapokuwa South Afrika.

Diamond ameandika maneno haya :
 “Jus decided to get this for my south african up and downs trip…..👍 #SideChick“


Serikali yatoa ajira kwa walimu 3,081.....Yasema upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati ni 60%...!!



Serikali imesema jumla ya walimu 3,081 wakiwemo walimu 7 wa shule ya Sekondari Omumwani Kagera, wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1.048 kati ya nafasi 4,129 za walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa kibali cha ajira.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa  akizungumza na Waandishi  Habari,ofsini kwake ambapo amewataka walimu wote walioajiriwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.
Amesema walimu walioajiriwa  wamepangwa moja kwa moja na TAMISEMI katika halmashauri zote nchini ambazo zina upugufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati.
Simbachawene amesema kati ya walimu hao walioajairiwa walimu 1,537 ni wa Shahada  na walimu 1,544 ni wa Stashahada.
“Sehemu kubwa ya walimu wa Shahada wamepangwa  kwenye shule za kidato cha tano na sita na wachache kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’ alisema.
Simbachawene amekiri  kuwa kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na Hisabati katika shule mbalimbali za sekondari nchini.
“Moja ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya sekondari ni upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati upungufu uliopo  katika shule 3,602 ni 26,026 sawa na asilimia 60.14 ya walimu 43,248 wanaohitajika” amesema Simbachawene
Amesema walimu wanaohitajika kwa masomo hayo ni walimu 43,248 lakini waliopo kwa sasa ni 17,252 pekee.
Amesema kwa sasa serikali ina shule za sekondari 3,602 na kati ya hizo shule 333 ni za kidato cha tano na sita huku zingine 54 za kidato cha tano zimeanzishwa .
Aidha amesema shule hizo za sekondari kwa upande wa masomo ya Sanaa ina ziada ya walimu 7,463 ambapo waliopo ni walimu 63,240 na wanaohitajika ni walimu 55,777.
“Kutokana na ziada hiyo ya walimu wa Sanaa serikali imeanza kuchukua hatua yawahamisha walimu hao katika shule za msingi ili kuziba upungufu wa walimu katika shule hizo’’ alisema

Stamina: Treni ya Umeme Dar Mpaka Moro Ikikamilika,Narudi Kuishi Zangu Moro..!!


Leo April 12 Rais Dkt John Pombe Magufuli amezindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli ambayo itakayorahisisha usafiri wa Dar es Salaam hadi Morogoro kwa njia ya treni.
Inawezekana mtu akawa anaishi Morogoro na kufanya kazi zake Da es Salaam kwani usafiri utakuwa wa uhakika na haraka zaidi. Rapper Stamina ambaye ni mzaliwa na Morogoro anayefanya mishe zake Dar, amehaidi kurudi kuishi Moro na wakati huo huo akiendelea kufanya mishe zake Dar endapo njia hiyo ya usafiri itaanza kufanya kazi.
“Ikikamilika hiyo Rais, naenda kuishi zangu Morogoro tu,” ameahidi Stamina wakati akipiga story na Prince Ramalove kupitia Kings Fm Leo.

Rais Magufuli Ampigia Simu MwanaFA na Kumwambia Anapenda Kazi Zake Hasa Wimbo wa Dume Suruali..!!!!!

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, jana amempigia simu Msanii wa Muziki wa kufokafoka aka Hip Hop ndugu Hamis Mwinjuma aka MwanaFalsafa aka MwanaFA aka Binamu, na kusema yeye ni mpenzi wa kazi zake haswa Wimbo wake unaotamba anga za Miziki wa #DumeSuruali ambao alimshirikisha Vanessa Mdee. Moja ya ya Msitari anaoupenda ni "Utoe hela kwani ina TV ndani?"
"Nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais Magufuli kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa #DumeSuruali" amesema MwanaFA kwenye Ukurasa wake wa Twitter

Jumanne, 11 Aprili 2017

Kuhusiana na Tetesi Kuwa Amelipwa Dola 5000 Ili Kusema Tofauti na Ukweli..Roma Kafunguka Haya Huku Akilia..!!!

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki amezungumza kwa hisia juu ya wasanii wenzake na watu wengine ambao wanahusisha kutekwa kwao na mchezo wa kiini macho.
“Watu wanasema tunatumika kisiasa tunataka kuichafua Serikali, wapo wanaosema tunatafuta kiki na kuna wengine wamekwenda mbali zaidi na kudai tumelipwa Dola 5,000 ili tutengeneze habari hii.
“Tunaumizwa sana na kauli hizo, nguvu za watu walizotumia kupaza sauti zao halafu watu wanasema tunacheza mchezo, hatuwezi kuhatarisha maisha yetu kwa sababu ya fedha sisi ni watu wa kawaida sana familia zetu ni masikini, lakini hatuwezi kukubali kuumizwa hivi kwa ajili ya fedha.”
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema anataka kupata majibu ya tukio la utekaji wa Roma Mkatoliki kabla ya kuwasilisha bajeti yake bungeni.
“Mimi nitakuwa kwa wapelelezi, nataka kujua suala hili nipate majibu kabla sijawasilisha bajeti yangu bungeni ili bajeti yangu ipite bila makelele mengi,” amesema.